MAFANIKIO YA TAN WARRIORS SPORTS ACADEMY NCHINI ITALIA , TAZAMA WALIVYOTUA NCHINI KWA KISHINDO

MAFANIKIO YA TAN WARRIORS SPORTS ACADEMY NCHINI ITALIA , TAZAMA WALIVYOTUA NCHINI KWA KISHINDO

Tan Warriors Sports Academy ya mkoani Morogoro inayojihusisha na kuwaendeleza Vijana katika mpira wa Miguu , Basketball , Riadha n.k Leo Julai 16 , imerejea nchini ikitokea Italy ambapo ilienda tangu June , 20 mwaka huu kushiriki michuano ya Shirikisho la Michezo ya Vyuo Vikuu kwa mwaliko wa Chuo Kikuu cha Kamerino kilichopo nchini Italy.

Wakizungumza na Waandishi wa habari mapema leo hii katika eneo la bandari Jijini Dar Es Salaam wakitokea Zanzibar walipofikia hapo Jana Viongozi hao wamesema Safari yao ya Takribani wiki kadhaa nchini Italia imekua ya mafanikio makubwa kwa Academy yao na kwa vijana wao pia maana wamejifunza vitu vingi ambavyo vinaenda kubadilisha kabisa academy iyo

” Safari hii imekua ya Mafanikio makubwa vijana wamerudi salama na kwa mafanikio ni mazuri kwa vijana wote tulioondoka nao . tuliondoka na vijana sita ( Watatu Basketball na watatu Football ) , Vijana wameipeperusha bendera ya nchi yetu , pia Vijana walipata nafasi ya kufanyiwa majaribio katika vilabu tofautitofauti kwakweli walifanya vizuri sana na tutegemee mazuri maana wanahitajika tena kurudi kwenye vilabu kwa awamu ya Pili kwa maana vilabu hivyo vimetupa ofa ya kupeleka wanafunzi zaidi ” Alisema Bwn. Sulleiman Khalid – Technical Director wa TAN WARRIOURS SPORTS ACADEMY .

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Translate »