Rais Mwinyi ameitangaza rasmi kesho Jumatano siku ya mapumziko Kitaifa Zanzibar.

Rais Mwinyi ameitangaza rasmi kesho Jumatano siku ya mapumziko Kitaifa Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema kwa mara ya kwanza Maadhimisho ya siku ya Mwaka mpya wa Kiislamu;Mwaka 1445 Hijriya kutambuliwa na Serikali kuwa ni siku ya mapumziko. Serikali imekubali ombi la Waislamu kuhusu kuiadhimisha siku hii na kuwa ya mapumziko kwa madhumuni ya kuipa hadhi na

Inaweza kuwa picha ya Watu 9
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1, jukwaa na maandishi
Inaweza kuwa picha ya Watu 6, jukwaa na maandishi yanayosema 'KILELE CHA MAADHIMISHO YA MWAKA MPYA WA KIISLAM ZANZIBAR 1445-H'
Inaweza kuwa picha ya jukwaa na maandishi
Inaweza kuwa picha ya Watu 5, jukwaa na maandishi
Inaweza kuwa picha ya Watu 3, jukwaa na maandishi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema kwa mara ya kwanza Maadhimisho ya siku ya Mwaka mpya wa Kiislamu;Mwaka 1445 Hijriya kutambuliwa na Serikali kuwa ni siku ya mapumziko.

Serikali imekubali ombi la Waislamu kuhusu kuiadhimisha siku hii na kuwa ya mapumziko kwa madhumuni ya kuipa hadhi na kuiongezea hamasa siku ya mwaka mpya wa Kiislamu kila inapofika.

Ameyasema hayo leo katika hafla ya Maadhimisho ya kuukaribisha kuingia mwaka mpya wa Kiislamu yaliyofanyika Msikiti wa Munawar Mfikiwa, Wilaya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba.

Kwa Mamlaka ya kikatiba chini ya kifungu 6(1)(a)cha Sheria ya Masuala ya Rais wa Zanzibar,Namba:3 ya 2020, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi ameitangaza rasmi kesho Jumatano itakuwa ni siku ya mapumziko Kitaifa Zanzibar.

Aidha, Rais Alhajj Dk.Mwinyi ametoa wito kwa Wazazi na Walezi kutimiza wajibu wa malezi ya vijana kuwa na kizazi chema chenye kumjua Mwenyezi Mungu kwa kutekeleza maarimsho yake na kujiepusha na makatazo katika misingi bora ya maadili kwa mujibu silka na tamaduni za dini.

Vilevile, kuwa raia wema na wazalendo wa kuijenga nchi kwa kuendelea kudumisha amani iliyopo kwa kila mmoja.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Translate »