Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi amewataka waumini wa dini ya kiislamu kuzingatia umuhimu wa suala la elimu. Ameyasema hayo leo baada ya sala ya ijumaa katika msikiti wa Abuu Ubadya uliopo Fuoni Meli Saba Mkoa wa Mjini Magharibi. Alhaj. Dk. Mwinyi amewataka wazazi kuwahimiza watoto wao kusoma




Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi amewataka waumini wa dini ya kiislamu kuzingatia umuhimu wa suala la elimu.
Ameyasema hayo leo baada ya sala ya ijumaa katika msikiti wa Abuu Ubadya uliopo Fuoni Meli Saba Mkoa wa Mjini Magharibi.
Alhaj. Dk. Mwinyi amewataka wazazi kuwahimiza watoto wao kusoma elimu zote mbili ikiwemo elimu ya dini na elimu ya dunia, kufanya hivyo itasaidia kuharakisha hatua za kimaendeleo.
Katika maelezo yake Alhaj Dk.Mwinyi amesema mataifa yaliyoendelea kwa kiasi kikubwa wamewekeza fedha nyingi kwenye elimuya utafiti kutokana na kuwa elimu ndio inayoleta mafanikio.
Mbali na hilo Rais Dk.Mwinyi amesema moja ya sababu kuu za mmomonyoko wa maadili katika jamii hutokana na ukosefu wa elimu.