Waziri Soraga Atoa Rai Kuwekeza kwa Walimu ili Kuboresha Rasilimali Watu

Waziri Soraga Atoa Rai Kuwekeza kwa Walimu ili Kuboresha Rasilimali Watu

Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais (Kazi, Uchumi na Uwekezaji) Zanzibar, Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga ametoa rai ya kuendelea kuwawezesha na kuwajengea uwezo Walimu nchini ili wawe walimu wenye uwezo na ujuzi wa kutosha, hivyo kutoa elimu inayokusudiwa itakayoweza kuboresha rasilimali watu. Ameyasema hayo mapema leo jijini Dar es Salaam katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa

Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais (Kazi, Uchumi na Uwekezaji) Zanzibar, Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga ametoa rai ya kuendelea kuwawezesha na kuwajengea uwezo Walimu nchini ili wawe walimu wenye uwezo na ujuzi wa kutosha, hivyo kutoa elimu inayokusudiwa itakayoweza kuboresha rasilimali watu. Ameyasema hayo mapema leo jijini Dar es Salaam katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere wakati akihojiwa mubashara na kituo cha televisheni cha Clouds  kuhusu Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika Kuhusu Mtaji Rasilimali Watu unaoendelea jijini humo. “Ni kweli tunajenga miundombinu ya elimu, lakini tusisahau suala zima la kutoa mafunzo kwa Walimu wetu. Suala hili ni la msingi kwa sababu unaweza kuwa na miundombinu mizuri lakini kama hakuna Walimu bora, hizo juhudi zingine zote hazitokuwa na tija”, alisema Waziri Soraga. Ameyataja mambo matatu makubwa ambayo lazima yaangaliwe ili kuboresha elimu ikiwemo; kuwekeza katika Walimu bora kwa kuwapa mafunzo na motisha za kutosha, kuangalia mitaala ya elimu kama inakwenda sambamba na uhalisia wa uchumi ambao nchi inakwenda nao na la tatu ni kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya kuboresha elimu. “Ualimu ndio kada ambayo nchi inaitumia kujenga msingi wa taifa la kesho, hivyo kwa namna yoyote, ni lazima tuboreshe mazingira yao”, ameongeza Soraga. Amefafanua kuwa muamko ambao tayari umejengwa katika mkutano huu, umewafanya viongozi kupata ufahamu kwamba panapotakiwa kuendeleza nchi, kuna suala la kuwekeza kwenye miundombinu pamoja na rasilimali watu. Amemaliza kwa kusema kuwa, baada ya kusainiwa kwa Azimio la Dar es Salaam ambalo litakuwa ndio mwelekeo wa bara la Afrika katika suala la rasilimali watu, ni muhimu kwa viongozi wote kuona namna ya kujipanga kuliweka azimio hilo katika uhalisia.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Translate »