AJALI YAUA WANNE WA FAMILIA MOJA CHALINZE

AJALI YAUA WANNE WA FAMILIA MOJA CHALINZE

Jeshi la Polisi Mkoani Pwani limethibitisha vifo vya Watu wanne (Ndugu wa Familia moja) ambao wamefariki baada ya gari aina ya Toyota Prado walilokuwa wamepanda wakitokea Dar es salaam kwenda Same, Kilimanjaro kugongana uso kwa uso na Scania lililokuwa linatokea Arusha kwenda Dar es salaam. RPC wa Pwani Piusi Lutumo amesema ajali imetokea saa nane

Jeshi la Polisi Mkoani Pwani limethibitisha vifo vya Watu wanne (Ndugu wa Familia moja) ambao wamefariki baada ya gari aina ya Toyota Prado walilokuwa wamepanda wakitokea Dar es salaam kwenda Same, Kilimanjaro kugongana uso kwa uso na Scania lililokuwa linatokea Arusha kwenda Dar es salaam.

RPC wa Pwani Piusi Lutumo amesema ajali imetokea saa nane usiku wa kuamkia leo eneo la Mapatano Kata ya Mbwewe Halmashauri ya Chalinze Mkoani Pwani na waliofariki ni Dereva wa Prado Neech Msuya (45-50), Mfanyakazi wa Benki ya ABSA na Mkazi wa Dar es salaam pamoja na Watu watatu waliokuwa kwenye gari hilo ambao ni Dayana Mageta(40-45), Norah Msuya (40-45) na Ndugu mwingine wa kike.

Kamanda Lutumo amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Toyota Prado ambaye alihama upande wake na kugongana uso kwa uso na Scania “Mili ya marehemu wote imehifadhiwa katika Zahanati ya Lugoba kwa ajili ya uchunguzi na kutambuliwa na Ndugu”

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »