Rais Mwinyi Amekutana na Makamu wa Rais wa Uganda.

Rais Mwinyi Amekutana na Makamu wa Rais wa Uganda.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk Hussein Ali Mwinyi akimaliza ziara yake nchini Cuba, amekutana na Makamu wa Rais wa Uganda Mhe. Jessica Alupo pamoja na ujumbe wa Wizara ya Kilimo ya Cuba ikiongozwa na Naibu wa Wizara huyo Mhe. Bernado. Rais Dk Mwinyi katika mazungumzo hayo alimshawishi Makamu huyo

Inaweza kuwa picha ya Watu 12
Inaweza kuwa picha ya Watu 9 na jukwaa
Inaweza kuwa picha ya Watu 4, chumba cha habari, jukwaa na maandishi
Inaweza kuwa picha ya Watu 11
Inaweza kuwa picha ya Watu 5
Inaweza kuwa picha ya Watu 6 na meza

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk Hussein Ali Mwinyi akimaliza ziara yake nchini Cuba, amekutana na Makamu wa Rais wa Uganda Mhe. Jessica Alupo pamoja na ujumbe wa Wizara ya Kilimo ya Cuba ikiongozwa na Naibu wa Wizara huyo Mhe. Bernado.


Rais Dk Mwinyi katika mazungumzo hayo alimshawishi Makamu huyo wa Rais wa Uganda nchi yake ianze kutumia viuadudu, dawa inayotengenezwa Kibaha, Mkoa wa Pwani, Tanzania na kiwanda kinachotumia teknolojia kutoka kwa wataalamu wa Cuba kwa ajili ya kuangamiza vimelea vya mbu kwa lengo la kuangamiza Malaria.


Mhe. Rais Dk. Mwinyi alimueleza Makamu huyo wa Rais wa Uganda kwamba kiwanda hicho kilianza uzalishaji wa viuadudu tangu mwaka 2017.


Nchi kadha za Afrika zimenufaika na dawa hiyo ya viuadudu kutoka Kibaha ikiwemo Niger, Angola, Msumbiji na Eswatini.


Dk. Mwinyi alimueleza Makamu Jessica Alupo kwamba mbali ya kutengeneza viuadudu kiwanda hicho teknolojia yake kinaweza kutengeneza pia mbolea.
Baada ya Maelezo hayo Makamu wa Rais wa Uganda alionesha kuvutiwa na bidhaa hiyo na kueleza kwa vile nchi yake inasumbuliwa na Malaria wapo tayari kutumia bidhaa hiyo itakayosaidia kuondokana na vifo vya watoto na kina mama vinavyotokana na Malaria.


Kwa niaba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Rais Dk. Mwinyi aliahidi kuigaiya bure Uganda lita elfu moja za dawa hiyo waijaribu na baadae wapeleke wataalam wao wa Afya kuangalia teknolojia ya kuzalisha dawa hiyo ombi lililokubaliwa na Makamu wa Rais wa Uganda Jessica Alupo.


Naye Naibu Waziri wa Kilimo wa Cuba Mhe Bernado alieleza wamesaidia kuingiza teknolojia ya dawa ya viuadudu ili kusaidia mapambano dhidi ya Malaria Afrika.


Mazungumzo hayo pia yalihudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Steve Byabato na Balozi wa Tanzania nchini Cuba Mhe. Humphrey Polepole.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »