TUMIENI HUDUMA ZA JAMII ZINAZOTOLEWA BURE NA JESHI LA POLISI.

TUMIENI HUDUMA ZA JAMII ZINAZOTOLEWA BURE NA JESHI LA POLISI.

Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. HAMAD KHAMIS HAMAD amewataka wananchi kisiwani Pemba kutumia huduma za Jamii zikiwemo za Elimu na Afya zinazotolewa bure na Polisi kwa kushirikiana na Jumuiya ya Kuhamasisha Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii Pemba (JUKUMAKIKIPE) inayosimamiwa na Raia kutoka Korea. Akikagua Vituo vya Kutolea huduma hizo Kambi ya Polisi Madungu, Katika Wilaya

Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. HAMAD KHAMIS HAMAD amewataka wananchi kisiwani Pemba kutumia huduma za Jamii zikiwemo za Elimu na Afya zinazotolewa bure na Polisi kwa kushirikiana na Jumuiya ya Kuhamasisha Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii Pemba (JUKUMAKIKIPE) inayosimamiwa na Raia kutoka Korea.

Akikagua Vituo vya Kutolea huduma hizo Kambi ya Polisi Madungu, Katika Wilaya ya Chake chake, Mkoa wa Kusini Pemba amesema Mwitikio bado ni mdogo kwa wananchi kujitokeza kutumia huduma hizo hivyo amewaasa Wananchi na Askari wa Jeshi hilo kutumia fursa hizo kwa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP. ABDALLA HUSSEIN MUSSA ameeleza kuwa huduma zinazotolewa Vituoni hapo kwa wananchi wachache waliojitokeza ni Elimu kwa kutumia vifaa vya kisasa, Tiba kwa maradhi mbalimbali na Michezo.

Nae BETRIS MPARO wa Jumuiya ya Kuhamasisha Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii Pemba, kwa niaba ya Jumuiya hiyo amelishukuru Jeshi la Polisi kwa ushirikiano wanaoupata kutoka kwa watendaji wa Jeshi hilo.

NA OMAR HASSAN –

ZANZIBAR 22/09/2023

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Translate »