Nitaimarisha Sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Nitaimarisha Sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amejipanga kuziimarisha Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo ili kuhakikisha matarajio ya Serikali na wananchi kutoka kwenye Wizara hiyo yanafikiwa. Msigwa ameyasema hayo leo Septemba 29, 2023 jijini Dodoma wakati akikabidhiwa ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mhe. Balozi Saidi Yakubu ambapo

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amejipanga kuziimarisha Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo ili kuhakikisha matarajio ya Serikali na wananchi kutoka kwenye Wizara hiyo yanafikiwa.

Msigwa ameyasema hayo leo Septemba 29, 2023 jijini Dodoma wakati akikabidhiwa ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mhe. Balozi Saidi Yakubu ambapo ametaja kipaumbele chake cha kwanza kwenye wizara hiyo kuwa ni kuhakikisha anaziongezea sekta hizo kasi, ubunifu na kuleta matokeo chanya kwa wananchi.

“Watanzania wanahitaji furaha na hii ndio wizara ambayo inasimamia utekelezaji wa sera zinazowawezesha kupata furaha, hivyo nimejiandaa kuhakikisha maeneo yote katika sekta hizi tatu yanakwenda kwa kasi zaidi, nguvu, ari na ubunifu mkubwa”, alisema Msigwa.

Akizungumzia kuhusu michezo, Msigwa amesema kwenye wizara hiyo kuna majukumu mazito ikiwemo maandalizi ya Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) yanayotarajiwa kufanyika mwaka 2027 ambapo Tanzania, Kenya na Uganda ni waandaji wa mashindano hayo.

“Kwangu hili ni jukumu la kwanza kubwa ambalo ninapaswa mimi pamoja na viongozi wenzangu wa Wizara tulisimamie kwa nguvu zote ili matarajio ya maandalizi ya mashindano hayo yafanyike vile yanavyotakiwa. Ni lazima jambo hili lifanyike kwa mafanikio makubwa”,  alisisitiza Msigwa.

Katika Sekta ya Utamaduni, Msigwa amesema kuwa Tanzania ina mambo mengi yanayohusu sekta ya utamaduni ambapo mtazamo wake ni kujenga taasisi imara zinazosimamia utamaduni kama ambavyo imefanyika kwa kiasi kwenye Sanaa na Michezo. Vilevile, ataangalia upande wa miundombinu kwani ni vigumu kutekeleza majukumu yaliyopangwa kama hakuna miundombinu inayotakiwa.

“Tutaangalia miundombinu tuliyonayo kwamba ni kiasi gani inatuwezesha kusaidia kukuza na kuubidhaisha utamaduni, tutaangalia utamaduni kama utambulisho wa nchi na moja kati ya bidhaa zinazotakiwa kuleta fedha kwa Watanzania”, alisema Msigwa.

 Wakati akikabidhi ofisi hiyo,  Mhe.  Balozi Yakubu ametoa wito kwa watumishi wa wizara hiyo wajitume zaidi na kutoa ushirikiano kwa Katibu Mkuu, Gerson Msigwa ili kuweza kusukuma gurudumu l

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Translate »