Baraza la Maulidi simamieni miongozo mizuri ya usomwaji wa maulidi.

Baraza la Maulidi simamieni miongozo mizuri ya usomwaji wa maulidi.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amalitaka Baraza la Maulidi Zanzibar kuendelea kusimamia na kutoa maelekezo na miongozo mizuri ya usomwaji wa maulidi nchini kwa kwani kwa kiasi kikubwa maadili yamekiukwa kwa miaka ya karibuni. Ahaj Dk. Mwinyi aliyasema hayo alipozungumza kwenye hafla ya Baraza la Maulid Zanzibar, Ukumbi

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amalitaka Baraza la Maulidi Zanzibar kuendelea kusimamia na kutoa maelekezo na miongozo mizuri ya usomwaji wa maulidi nchini kwa kwani kwa kiasi kikubwa maadili yamekiukwa kwa miaka ya karibuni.

Ahaj Dk. Mwinyi aliyasema hayo alipozungumza kwenye hafla ya Baraza la Maulid Zanzibar, Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil, Mkoa wa Mjini Magharibi

Alisema, Baraza la Maulid Zanzibar litasaidi kurejesha misingi sahihi ya usomwaji bora wa Maulid kwa kuwatumia wanazuoni wa ndani na nje ya nchi.

Alhaj Dk. Mwini alieleza, sherehe za mazazi ya Mtume S.A.W zinafaida kiuchumi na jamii mbali na kukuza umoja wa jamii na maeneo kwa watu kualikana kutoka maeneo mablimbali hali iliyochangia kwa kiasai kikubwa kukuza mahusiano na biashara.

Alisema, historia ya Mwambao wa Afika Mashariki imedhihirisha kukua kwa mahusiano yaliyochangiwa kuimarika kwa watu wa maeneo tofauti kualikana mihadhara ya maulidi jambo lililochangia kukuza ushirikiano na kuanzishwa biashamba mbalimbali baina yao na manufaa makubwa yalipatikana kwa jamii kubasilishana mila na silka njema.

Alisema, Zanzibar kuliwahi kuishi masheikh wakubwa waliotokana na mialiko ya maulidi kutoka maeneo mbalimbali ya mwambao na wengine wakitokea nchi za Oman, Yemen, Komoro ambao walitoa mchango mkubwa kwa Zanzibar.

Pia, alieleza usomwaji wa maulidi unakwenda sambamba na mazazi ya Mtume S.A.W kama yalivyofanywa na wanazuoni waliopita kwa kuzingatia maadili ya kiislam

Alhaj Dk. Mwinyi aliipongeza Ofisi ya mufti Zanzibar kwa kusimamia vyema kusimiamia na kuratibu shughuli mbalimbali za dini na kusimamia maadili ya vijana.

Vile vile alieleza Maratajio ya Serikali kwa Baraza hilo la Maulid litasaidia ni kuwaunganisha waumini wa Kiislamu kutoka maeneo mbalimbali ya nchi kuisoma vizuri Sira na mwenendo mzuri wa Mtume S.AW ili kujenga misingi bora ya kuendesha shughuli za Maulid.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Maulidi ambae pia ni Kaadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Hassan Othman Ngwali aliitaka jamii kuendelea kumshiba Mtume (SAW) kwenye maisha yao yote kwa kufuata yote maarisho yake na kuyaacha makatazo yake ili kuepukana na matendo maovu yakiwemo udhalilishaji na ya upotevu wa maadili.

Naye, Sheikh Khalid Mfaume, Katibu wa Ofisi ya Mufti aliitaka jamii kuendelea kusheherekea Mauli ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad SAW kwa nidhamu, heshma na mila na silha za dini ya Kiislam kwa kuepuka michanganyiko na miingiliano ya waumini wananwake na wanaume kwenye eneo moja.

Aidha alisifu kuimarika kwa shughuli za dini ya Kiislam Zanzibar kwa kuendelea kupata baraka za kiongozi wa mkuu wan chi, Alhaj Rais Dk. Hussein Mwinyi ambae alisifu jitihada zake za kushirikia na waumini mbalimbali wa dini hiyo kwa nyakati tofauti kwenye maeneo yote ya Zanzibar.

Alisema Alhaj Dk. Mwinyi amekua kinara wa kuhimiza ibada kwa kujumuika nao kwenye Ibada za sala misikitini, kusali nao pamoja Taraweikh kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Kushirikiana nao vyema kwenye sherehe za mwaka mpya wa Kiislam 1445 H pamaja na sherehe za mazazi ya Mtume (S.A.W) yaliyofanyija juzi kwenye viwanja vya Maishara.

Kwaupande wake Sheikh Muhamad Hassan Al Habsy kutoka Yemen aliiusia jamii ya Wazanzibari kuendelea kuishi na matengo ya Mtume S.A.W kwa kutii na kumtukuza kwani uhakika wa dini na matendo yake ni kutoka kwa Allah (S.W).

Shughuli hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini na Serikali, akiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Alhaj Haroun Ali Suleiman, Waziri wa Ofisini ya Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Harusi Said, Katibu Mkuu kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Mhandis Zena Ahmed Suleiman, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Idriss Kitwana Mustafa na viongozi wengine.

IDARA YA MAWASILIANO IKULU, ZANZIBAR

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Translate »