Mke wa Rais Mariam Mwinyi akihutubia katika ufunguzi wa Jukwaa la nne la Viongozi Wanawake.

Mke wa Rais Mariam Mwinyi akihutubia katika ufunguzi wa Jukwaa la nne la Viongozi Wanawake.

Mke wa Rais wa Zanzibar , Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mhe.Mama Mariam Mwinyi ametoa rai kuwekeza katika elimu ya mtoto wa kike ili kumwezesha kiuchumi, kijamii husasan kujiamini kufanya maamuzi sahihi kuhusiana na afya ya uzazi na mpangilio kufikia maendeleo endelevu kwa kuzingatia uzazi

Mke wa Rais wa Zanzibar , Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mhe.Mama Mariam Mwinyi ametoa rai kuwekeza katika elimu ya mtoto wa kike ili kumwezesha kiuchumi, kijamii husasan kujiamini kufanya maamuzi sahihi kuhusiana na afya ya uzazi na mpangilio kufikia maendeleo endelevu kwa kuzingatia uzazi wa mpango na lishe bora kulingana na mahitaji ya idadi ya watu.

Mama Mariam Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 09 Oktoba 2023 akitoa salamu za nchi katika ufunguzi wa Jukwaa la nne la Viongozi Wanawake lililoandaliwa na Mke wa Rais wa Burundi Mhe. Angeline Ndayishimiye lililofanyika ukumbi wa Hoteli ya Kiriri , Bujumbura Burundi.

Jukwaa hilo limefunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Burundi Mhe.Gervais Ndirakubuca aliyemwakilisha Rais wa Burundi Mhe.Evariste Ndayishimiye.

Wengine waliohudhuria ni Mke wa Rais wa Kenya Mhe.Mama Rachel Ruto, Mke wa Rais wa Rwanda Mhe.Mama Jeannette Kagame pamoja na wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo wawakilishi wa Mashirika ya Umoja wa Afrika , kikanda , wadau wa maendeleo na ujumbe kutoka China.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Translate »