Wawekezaji Sekta Binafsi Waombwa Kuwekeza kwenye Shule za Mafunzo ya Amali.

Wawekezaji Sekta Binafsi Waombwa Kuwekeza kwenye Shule za Mafunzo ya Amali.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda amewaomba Wamiliki waShule zisizo za Serikali nchini kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu ya mafunzo ya amaliambayo Serikali ya Awamu ya Sita inatarajia kuyatilia mkazo kama mapendekezo ya Rasimuya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 toleo la 2023 na mabadiliko ya Mtaala waElimu ya

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda amewaomba Wamiliki wa
Shule zisizo za Serikali nchini kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu ya mafunzo ya amali
ambayo Serikali ya Awamu ya Sita inatarajia kuyatilia mkazo kama mapendekezo ya Rasimu
ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 toleo la 2023 na mabadiliko ya Mtaala wa
Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu yatapitishwa na Mamlaka husika.
Waziri Mkenda ameyasema hayo Oktoba 10, 2023 jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano
kati ya Wizara hiyo na Wamiliki wa Shule mbalimbali nchini.
Amesema kuwa, Serikali itajitahidi kwa kadri ya uwezo wake kuona ni kwa jinsi gani
watasaidia Sekta Binafsi ambao watapenda kuwekeza katika mkondo wa mafunzo ya amali
kwani Serikali pekee haitoweza kuanza kwa kasi kwa sababu lazima kuwe na uwekezaji wa
kutosha kwani ni dhahiri kuwa watu wataunyanyapaa mkondo wa mafunzo ya amali kama
utaanzishwa bila kuwekeza vya kutosha.
“Kuna baadhi ya Shule za Mafunzo ya Amali zipo, zingine tutazifufua, lakini tutaziongezea
zaidi. Tunapenda kuwahamasisha wawekezaji wanaohitaji kuwekeza kwenye sekta binafsi
wawekeze kwenye upande wa mafunzo ya amali, nawaomba tushikane mikono kwa pamoja
kwani tunawahitaji sana kuwekeza katika mkondo huu.” Amesema Prof. Mkenda.
Vile vile, amewashukuru Wamiliki wa shule mbalimbali nchini pamoja na wadau wa elimu
kwa kuwekeza katika ujenzi bora wa shule ambapo wameongeza fursa kwa wazazi kuchagua
ni wapi wawapeleke watoto wao kupata elimu bora hapa hapa nchini kwani zamani wengi
wao walikuwa wakisafiri hadi nje ya nchi kutafuta shule zilizo bora.
“Rais wetu Samia Suluhu Hassan kati ya vitu ambavyo vinamtambulisha ni kuweka msukumo
mkubwa na wepesi wa kufanya biashara na kukuza uwekezaji ivyo, katika kutekeleza
maelekezo ya Rais wetu tumeona tuwasikilize ili tufahamu ni nni tunatakiwa kukifanya
kuleta wepesi katika uwekezaji na uendeshaji wa shule zetu, nyie sio maadui wala
changamoto bali ninyi ni fursa na msaada mkubwa kwa Serikali katika kuimarisha elimu.”
Akifafanua kuhusu kuanza kutumika kwa mitaala mipya ya elimu, Waziri Mkenda amesema,
mitaala hiyo inatarajiwa kuanza Januari, 2024 kwani vitabu vya ziada na kiada vilivyopo bado
ni muhimu na vitatumika, kikubwa ni kuandaa Walimu ambao nao mabadiliko ya utoaji
mafunzo sio makubwa.
Amemalizia kwa kufafanua kuwa kama mapendekezo yatakayojadiliwa katika kikao hicho
yatapita kama yalivyokuwa, mitaala mipya itaanza kutumika kwa wanaoanza Shule ya
Msingi mpaka waliopo darasa la tatu ambao watakamilisha elimu ya msingi darasa la sita
lakini itakuwa ni lazima kuendelea na shule mpaka kidato cha nne, wengine watakaoanza na
mitaala hiyo ni Kidato cha Kwanza, Kidato cha Tano na Elimu ya Ualimu mwaka wa kwanza.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Translate »