SPIKA TULIA ACKSON RAIS WA MABUNGE DUNIANI.

SPIKA TULIA ACKSON RAIS WA MABUNGE DUNIANI.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb) akizungumza mara baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) katika uchaguzi uliofanyika tarehe 27 Oktoba, 2023 Jijini Luanda nchini Angola wakati wa Mkutano wa 147 wa Umoja huo. Mhe. Dkt Tulia alishinda uchaguzi huo mara baada ya

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb) akizungumza mara baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) katika uchaguzi uliofanyika tarehe 27 Oktoba, 2023 Jijini Luanda nchini Angola wakati wa Mkutano wa 147 wa Umoja huo.

Mhe. Dkt Tulia alishinda uchaguzi huo mara baada ya kupata kura 172 ambazo ni sawa na asilimia 57 ya kura 303 zilizopigwa na Wajumbe walioshiriki Mkutano wa 147 wa IPU.

Dkt. Tulia amewashinda wagombea wengine watatu waligombea nafasi hiyo ambao ni Mhe. Adji Diarra kutoka Bunge la Senegal aliyepata kura 59, Mhe. Catherine Hara Spika wa Bunge la Malawi aliyepata kura 61 na Mhe. Marwa Hagi kutoka Bunge la Somalia aliyepata kura 11.

Mhe. Dkt. Tulia anakuwa Rais wa 31 wa IPU na pia Mwanamke wa kwanza kutoka Bara la Afrika kushika wadhifa huo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »