WALIMU WANAOFUNDISHA KIINGEREZ,WAMETAKIWA KUSAMBAZA UJUZI WA SOMO HILO.

WALIMU WANAOFUNDISHA KIINGEREZ,WAMETAKIWA KUSAMBAZA UJUZI WA SOMO HILO.

Katibu tawala wa Mkoa wa Pwani Bw. Rashid Kassim Mchatta ametoa wito kwa Walimu wa msingi wa Somo la English kusambaza ujuzi wa somo hilo kwa wenzao hasa katika kipindi hiki ambacho Serikali inatarajia kutekeleza mtaala mpya ifikapo Januari 2024. Mchatta ametoa wito huo Novemba 22 alipofungua mafunzo ya kusimamia na kutekeleza muhtasari wa Somo

Katibu tawala wa Mkoa wa Pwani Bw. Rashid Kassim Mchatta ametoa wito kwa Walimu wa msingi wa Somo la English kusambaza ujuzi wa somo hilo kwa wenzao hasa katika kipindi hiki ambacho Serikali inatarajia kutekeleza mtaala mpya ifikapo Januari 2024.

Mchatta ametoa wito huo Novemba 22 alipofungua mafunzo ya kusimamia na kutekeleza muhtasari wa Somo la English kwa Shule za Msingi kulingana na Mtaala mpya wa Elimu ya Msingi unaotarajiwa kuanza kutekelezwa Januari 2024.

Amesema, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania na OR-TAMISEMI chini ya ufadhili wa Shirika la la Maendeleo la Uingereza UK-International Development kupitia mradi wa “Shule Bora” imeandaa Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini (MEWAKA) kuhusu Muhtasari wa Somo la English kulingana na mabadiliko makubwa yaliyofanyika katika mitaala mipya.

Aidha, Mchatta amesema, lengo la mafunzo haya ni kukuza uwezo wa walimu wa Somo la English wa Shule za Msingi kutekeleza Mtaala Mpya, kuimarisha umahiri wa washiriki katika kutumia mbinu shirikishi za ufundishaji na ujifunzaji wa Somo la English ili kuleta matokeo chanya kwa wanafunzi wote.

Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Pwani Bi. Sara Mlaki amesema, kupitia mafunzo haya kwa Walimu wa Msingi wa Somo la English katika Wilaya ya Chalinze yataenda kuleta mabadiliko chanya katika ufundishaji na ujifunzaji na kuongeza ufaulu hasa katika somo hilo.

Pia, Bi Mlaki amesisitiza walimu kupeleka ujuzi walioupata kwa walimu wengine ili iwe chachu ya kuongeza ufaulu katika Wilaya ya Chalinze hasa katika Somo la English.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »