WAZIRI MKUU AMEFUNGUA KONGAMANO LA WANAWAKE NA VIJANA KATIKA BIASHARA

WAZIRI MKUU AMEFUNGUA KONGAMANO LA WANAWAKE NA VIJANA KATIKA BIASHARA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Kongomano la Pili la Wanawake na Vijana Katika Biashara Adni ys Eneo Huru la Bara la Afrika (AFCTA )kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Kimataifa chaJulius Nyerere jijini Der es salaam, Disemba 6, 2023. Waziri Mkuu, KASSIM MAJALIWA akisindikizwa na Waziri

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Kongomano la Pili la Wanawake na Vijana Katika Biashara Adni ys Eneo Huru la Bara la Afrika (AFCTA )kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Kimataifa chaJulius Nyerere jijini Der es salaam, Disemba 6, 2023.

Waziri Mkuu, KASSIM MAJALIWA akisindikizwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji (kulia kwake ) pamoja na viongozi wengeine wakati alipotoka kwenye  Kituo cha mikutano cha  Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Der es salaam kufungua   Kongomano la Pili la Wanawake na Vijana Katika Biashara Ndani ya Eneo Huru la Bara la Afrika (AFCTA )kwenye Kituo cha  Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Der es salaam, Disemba 6, 2023.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na viongozi baada ya kufungua  kufungua   Kongomano la Pili la Wanawake na Vijana Katika Biashara Ndani ya Eneo Huru la Bara la Afrika (AFCTA ) kwenye Kituo cha  Mikutano cha Kimataifa chaJulius Nyerere jijini Der es salaam, Disemba 6, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama nyuzi za mkonge wakati alipotembelea banda la maonesho la kampuni ya AJA Tanzania Limited inayojishugulisha na Biashara ya nyuzi za mkonge na bidhaa zake kabla ya kufungua   Kongomano la Pili la Wanawake na Vijana Katika Biashara Ndani ya Eneo Huru la Bara la Afrika (AFCTA ) kwenye Kituo cha  Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Der es salaam, Disemba 6, 2023. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Happiness Nyiti na kulia ni Ofisa  Mtendaji Mkuu  wa kampuni ya Mwnamama Soko, Dorris Malle

Baadhi ya washiriki  wa Kongomano la Pili la Wanawake na Vijana Katika Biashara Ndani ya Eneo Huru la Bara la Afrika (AFCTA) kwenye Kituo  cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Der es salaam, Disemba 6, 2023.

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka washiriki wa kongamano la Pili la Wanawake katika Biashara ndani ya Eneo Huru la Biashara Barani Afrika kujadili namna ya kuwezesha ushiriki imara wa wanawake katika biashara ndani ya bara la Afrika.

“Ni muhimu sana katika kongamano hili mkaja na mipango mahsusi ya hatua zinazotakiwa kuchukuliwa na kuimarisha ushirikiano kwa lengo la kuwa na ushiriki wenye tija kwa wanawake katika biashara unakamilishwa”

Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo (Jumatano, Desemba 6, 2023) alipomuwakilisha Rais Dkt. Samia  katika ufunguzi wa Kongamano hilo linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa kufanyika kwa Kongamano hili kwa mara ya pili ni ishara tosha ya kuonyesha dhamira ya Nchi Washiriki wa Eneo Huru la Biashara Barani Afrika kukuza ushiriki wa wanawake katika biashara chini ya Eneo Huru la Biashara Barani Afrika.

“Kufanyika kwa Makongamano haya kunatoa nafasi muhimu kwa wadau mbalimbali wa kuwawezesha wanawake kujadiliana na kutafuta ufumbuzi wa pamoja wa changamoto zinazokwamisha jitihada za wanawake katika biashara”

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa miongoni mwa faida za kuwa na Eneo Huru la Biashara la Barani Afrika ni kusaidia kuongezeka kwa biashara baina ya nchi za Afrika kutokana na nchi kuondoleana ushuru wa forodha “Faida Nyingine ni kushughulikia kwa pamoja vikwazo vya biashara visivyo vya kodi na kukuza uongezaji thamani wa malighafi zinazozalishwa ndani ya Afrika”

Katika hatua nyingine Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imeanzisha Mfumo Rahisi wa Biashara (Simplified Trade Regime – STR) kwa ajili ya mauzo ya nje ya mipakani kwa ajili ya kuwasaidia wafanyabiashara wadogo kwa mipakani. 

Mheshimiwa Majaliwa amesema uamuzi wa kuazisha mfumo umeonesha dhamara ya jumuiya hiyo katika kutambua ushiriki mkubwa wa wanawake kwenye biashara ndogo ndogo za mipakani.

Naye Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa kampuni nane za Kitanzania zimeanza kufanya biashara na zimepeleka biashara mara 17 kwenye nchi tano zilizopo katika ndani ya Eneo Huru la Biashara Barani Afrika

Amesema baadhi ya kampuni hizo ni Ajat ltd, Mama Mia’s Soko na NatureRipe zote za nchini Tanzania na zinamilikiwa na wanawake. “Tutaendelea kufanya kazi kwa karibu na sekta binfsi na kushughulikia  kero zote ili tuendelee kuwainua Wakawake”

Kwa upande wake, Waziri wa Menendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Doroth Gwajima amesema uwezeshaji wanawake na vijana kiuchumi ni miongoni mwa vipaumbele vya Serikali ili kuleta usawa wa kijinsia na hivyo kufikia maendeleo jumuishi na endelevu.

“Katika kufikia adhma hiyo serikali imetidhia na inatekeleza mkataba na maazio ya kikanda na kimataifa ikiwemo mkataba wa eneo huru barani afrika ambao unatoa fursa za kiuchumi kwa wanawake na hata wanaume ndani ya bara letu”.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

JUMATANO, DESEMBA 06, 2023.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »