TUPENDANE, TUSHIKAMANE NA TUDUMISHE AMANI.

TUPENDANE, TUSHIKAMANE NA TUDUMISHE AMANI.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi amewaomba wananchi kuendelea kushikamana, kuwa wamoja, kudumisha amani na utulivu ili kuzidi kupiga hatua ya maendeleo ya uchumi na ustawi wa jamii nchini. Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Dua ya kumuombea Mwanachuoni mkubwa Zanzibar Alhabyb

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi amewaomba wananchi kuendelea kushikamana, kuwa wamoja, kudumisha amani na utulivu ili kuzidi kupiga hatua ya maendeleo ya uchumi na ustawi wa jamii nchini.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Dua ya kumuombea Mwanachuoni mkubwa Zanzibar Alhabyb Ahmad Bin Abuubakar Bin Sumeit iliyofanyika Msikiti wa Ijumaa Malindi , Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 22 Aprili 2024.

Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa leo imemitimia miaka 102 tangu kufariki kwa Mwanachuoni Alhabyb Ahmad Bin Abuubakar Bin Sumeit amemuombea kwa Mwenyezi Mungu amrehemu na Wanazuoni wengine.

Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi ameishukuru na kuipongeza Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar kwa kuendelea kuratibu shughuli za Dini na kuzisimamia.

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amesema jukumu la kuwaombea Dua Waislamu waliotangulia ni la kila Muumini wa Dini hiyo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Translate »