Idara ya uhamiaji mkoa wa Kigoma imewakamata raia wa kigeni 52 kutoka nchi ya Burundi na jamuhuri ya kidemokrasia ya kongo walioingia nchini bila vibali pamoja na kuwakamata watanzania 3 waliokuwa wakijihusisha na kuwatumikisha baadhi ya raia hao. Miongoni mwa waliokamatwa wapo wakimbizi 12 waliotoroka katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilaya ya Kasulu. Akizungumzia hatua
Idara ya uhamiaji mkoa wa Kigoma imewakamata raia wa kigeni 52 kutoka nchi ya Burundi na jamuhuri ya kidemokrasia ya kongo walioingia nchini bila vibali pamoja na kuwakamata watanzania 3 waliokuwa wakijihusisha na kuwatumikisha baadhi ya raia hao.
Miongoni mwa waliokamatwa wapo wakimbizi 12 waliotoroka katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilaya ya Kasulu.
Akizungumzia hatua hiyo kaimu ofisa uhamiaji mkoa wa Kigoma Kamishna msaidizi wa uhamiaji Augustino Matheo amesema mnamo February 05 na 06 msako ulifanyika katika maeneo mbalimbali mkoani Kigoma nakufanikiwa kukamata raia 43 kutoka nchi ya Burundi kati yao wakiwemo wakimbizi 3 na raia 9 kutoka nchi ya kidemokrasia ya Kongo ambao ni wakimbizi kutoka kambi ya Nyarugusu.
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *