SERIKALI YATUMIA NGUVU KUWAANDIKISHA WATOTO WALIOZUILIWA KWENDA SHULE NA BABA YAO Mchungaji Marchades Mugishagwe Buberwa.

SERIKALI YATUMIA NGUVU KUWAANDIKISHA WATOTO WALIOZUILIWA KWENDA SHULE NA BABA YAO Mchungaji Marchades Mugishagwe Buberwa.

SERIKALI ya Wilaya ya Bukoba imefanikiwa kuwaandikisha shule watoto watatu waliozuiliwa kwenda shule na baba yao, Mchungaji Marchades Mugishagwe Buberwa. Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Deodatus Kinawiro akishirikiana na Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Bukoba, Dk Elipidius Baganda wamewandikisha watoto hao katika shule ya msingi Buyekera ambapo mtoto wa miaka 13 atasoma hatua ya lika

DEODATUS KINAWILI- MKUU WA WILAYA YA BUKOBA.
DK. ELIPIDIUS BAGANDA -AFISA ELIMU MSINGI MANISPAA YA BUKOBA.
Joselini miaka 13 darasa la tatu (MEMKWA) na kufanya mtihani wa darasa la nne, Joshua miaka tisa atasoma darasa la pili na Anna miaka mitano anaanza darasa la awali.
JACOBO KAIJAGE – MKUU WA SHULE YA MSINGI BUYEKERA.
AGRIPINA MAGAYA- MAMA MZAZI WA WATOTO.


SERIKALI ya Wilaya ya Bukoba imefanikiwa kuwaandikisha shule watoto watatu waliozuiliwa kwenda shule na baba yao, Mchungaji Marchades Mugishagwe Buberwa.

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Deodatus Kinawiro akishirikiana na Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Bukoba, Dk Elipidius Baganda wamewandikisha watoto hao katika shule ya msingi Buyekera ambapo mtoto wa miaka 13 atasoma hatua ya lika la kwanza darasa la tatu (MEMKWA) na kufanya mtihani wa darasa la nne, mtoto wa miaka tisa atasoma darasa la pili wakati mwenye umri wa miaka mitano atasoma darasa la awali.

Watoto hao wamezuiliwa kwenda shule na wazazi wao kwa ambao wanaamini kuwa elimu anayotakiwa kupewa mwanadamu ni Elimu ya kulijua neno la Mungu tuu,hivyo kuwaandikisha shule ni kwenda kinyume na maandiko ya Mungu kwenye Biblia Takatifu.

NA NYEMO MALECELA- KAGERA

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »