MPWAPWA WANZA KUGAGUA MABANGO, MAJENGO NA NYUMA KUTEKELEZA AGIZO LA SERIKALI LA UKUSANYWAJI WA KODI KUPITIA HALMASHAURI.

MPWAPWA WANZA KUGAGUA MABANGO, MAJENGO NA NYUMA KUTEKELEZA AGIZO LA SERIKALI LA UKUSANYWAJI WA KODI KUPITIA HALMASHAURI.

Mkuu wa wilaya ya mpwapwa mkoani Dodoma Jabir Shekimweri akiongozana na kamati yake ya ulinzi na usalama wakipita katika baadhi ya mitaa katika Kata ya mpwapwa mjini wakiangalia baadhi ya majengo ya nyumba baada ya serikali kuagiza kuanzia sasa kodi zote za majengo,mabango na vitambulisho vya wajasiliamali zitalipiwa kupita ofisi za halmashauri za wilaya ambapo

Mkuu wa wilaya ya mpwapwa mkoani Dodoma Jabir Shekimweri akiongozana na kamati yake ya ulinzi na usalama wakipita katika baadhi ya mitaa katika Kata ya mpwapwa mjini wakiangalia baadhi ya majengo ya nyumba baada ya serikali kuagiza kuanzia sasa kodi zote za majengo,mabango na vitambulisho vya wajasiliamali zitalipiwa kupita ofisi za halmashauri za wilaya ambapo awali zilikuwa zikikusanywa na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)
“Tumeamua kupita katika baadhi ya mitaa kuanga baadhi ya majengo ya wananchi wetu ambao sasa wameelekezwa kulipia kodi zao katika ofisi za halimashauri nakuna maelekezo tulipewa Kama wakuu wa wilaya na makatibu tawala wilaya na wakulugenzi wa halimashauri ya kuyafanyia kazi kabla ya February 28 mwaka huu hivyo Kama viongozi lazima tuyafanyie kazi kwa haraka maelekezo ya waziri wetu aliyotuelekeza”amesema shekimweri
Shekimweri amesema lazima tuangalie ubora wa majingo na kuwapatia elimu wananchi katika kujenga nyumba bora maana Kama Nyumba imejengwa kwa Matope haitalipiwa kodi pia kwa maeneo ya mijini lazima sasa wananchi wetu wabadilike na kujenga Nyumba bora na zinazoendana na ujio wa kimakao makuu kwakuwa serikali imeshahamia hapa Dodoma lazima wananchi nao wabadilike
Aidha shekimweri ameelezea kuwa Mamlaka za Serikali za Mitaa zina mtandao mkubwa kiutendaji hadi kwenye ngazi ya vitongoji kwa kuwa na wenyeviti wa vitongoji, vijiji na Mitaa na pia Kuna mabalozi hao huko wanawafahamu kila moja Kwa hiyo ni uamuzi wenye uelekeo wa ufanisi mkubwa kimakusanyo Kama tutawashirikisha viongozi wote na kwa uwazi mkubwa tutafanikiwa kukusanya kodi hizi kwa wakati
“Suala katika nidhamu ya uksanyaji na ujanjaujanja katika baadhi ya maeneo machache ni suala la kujipanga kiusimamizi Naamini ikitolewa elimu na uhamasishaji wa kutosha Jodi za majengo zitalipwa na watu wote ambao majengo Yao yatakadiriwa na kusajiliwa kwa mujibu wa sheria”amesema shekimweri
Serikali ngazi ya Wilaya tuko tayari kusimamia zoezi hili lenye umuhimu na tija mkubwa katika kutekeleza Bajeti za Serikali  na kuleta mafanikio zaidi kwenye miradi mikakati ya kitaifa na kiwilaya ambayo inatekelezwa kwa ukusanyaji wa kodi za wananchi
“Nitoe Rai kwa wananchi wa wilaya ya mpwapwa kuhakikisha wanalipa kodi kwa wakati ili pia serikali iwaletee huduma kwa wakati na niwaonye wale wachache wenyenye tabia ya kukwepa kulipa kodi kwa kipindi hichi cha serikali ya awamu ya tano hawana nafasi kabisa na tutawakamata wote wakwepa kodi na kuwashukulia hatua za kisheria katika vyombo husika”amesema shekimweri.

Na Barnabas kisengi Mpwapwa February  09 2021

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »