Serikali imeandaa kanuni mahususi zitakazotumika kusimamia udhibiti wa sekta ndogo ya fedha.

Serikali imeandaa kanuni mahususi zitakazotumika kusimamia udhibiti wa sekta ndogo ya fedha.

Serikali imesema kuwa tayari imeandaa kanuni mahususi zitakazotumika kwaajili ya usimamizi na udhibiti wa sekta ndogo ya fedha pamoja na kanuni za jumla kwaajili ya kutekeleza majukumu ya kisera ikiwa ni pamoja na kuhamasisha ,kusimamia na  kuendeleza sekta hiyo. Sekta ndogo ya fedha ni miongoni mwa huduma muhimu katika uchumi wa nchi kwani sekta hiyo

Serikali imesema kuwa tayari imeandaa kanuni mahususi zitakazotumika kwaajili ya usimamizi na udhibiti wa sekta ndogo ya fedha pamoja na kanuni za jumla kwaajili ya kutekeleza majukumu ya kisera ikiwa ni pamoja na kuhamasisha ,kusimamia na  kuendeleza sekta hiyo.

Sekta ndogo ya fedha ni miongoni mwa huduma muhimu katika uchumi wa nchi kwani sekta hiyo hutoa huduma za fedha kwa wananchi wa kipato cha chini kwa lengo la kuongeza kipato na kuchangia katika kukuza uchumi.

Akifungua Mafunzo ya Waratibu  wa Huduma za Biashara ndogo za fedha leo Jijini Dodoma  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango anayeshughulikia sera Adolf  Ndunguru ,amesema kutokana na umuhimu wa sekta hiyo serikali kupitia wizara hiyo ilifanya mapitio ya  sera ya Taifa ya huduma ndogo za fedha  mwaka 2000 na kutunga sera mpya ya 2017 pamoja na mkakati wa utekelezaji wake kwa kipindi cha miaka 10 ambayo ilianza  2017/2018-2027/2028.

Aidha, amesema ili kutatua changamoto zinazoikabili sekta ndogo ya fedha serikali ilitunga sheria ya huduma ndogo za fedha ya mwaka 2018 ili kuzitambua taasisi hizo ndogo za fedha katika madaraja manne ,kuboredha usimamizi na uendelezaji wa sekta hiyo nchini,kuipa mamlaka Benki kuu ya Tanzania kusimamia biashara ya huduma ndogo za fedha,kuwalinda watumiaji wa huduma hizo pamoja kudhibiti changamoto zinaweza kutokea katika sekta hiyo huku akitoa wito kwa waratibu walio hudhuria katika mafunzo hayo na hapa anabainisha zaidi.

Kwa upande wake  Dkt Charles Mwamaja ambaye ni kamishna wa Idara ya Maendeleo ya Sekta ya fedha amesema lengo la mafunzo hayo ni kujenga uelewa kwa waratibu wa huduma ndogo za fedha katika ngazi za Wizara,Mikoa na Halmashauri ili waweze ili wawezekutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa Sera, Sheria na Kanuni za Huduma Ndogo za Fedha pamoja na majukumu mengine kamaya ilivyoainishwa katika Kanuni za Huduma Ndogo za Fedha (Majukumu ya Waziri) za mwaka 2019.

Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango ilifanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Huduma ndogo za fedha ya mwaka 2000 na kutunga sera ya Taifa ya huduma ndogo za fedha ya mwaka 2017 na katika lengo la kutekelza sera hiyo serikali ilitunga sheria ya huduma ndogo za fedha mwaka 2018 ikifuatiwa na kanuni zake 2019 lengo likiwa ni kuweka mazingira wezeshi ya usimamizi na  uendelezaji wa sekta ya ndogo ya fedha nchini ili kuondoa changamoto zilikuwepo kwenye sekta hiyo na kuongeza mchango wake katika kukuza uchumi na kuondoa umasikini. 

Na Barnabas kisengi DODOMA.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »