Mwanasiasa Mkongwe Baraka Mohamed shamte amesema Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Huseein Ali Mwinyi atashinda vita ya kupigania maendeleo na kujenga uchumi imara. Pia amemtaja kiongozi huyo amezitumia vyema siku mia moja huku serikali yake ikisaini mikataba mikubwa ya kiuchumi . Hayo yameelezwa na Mwanasiasa huyo mashuhuri akimtaja Rais Dkt Mwinyi
Mwanasiasa Mkongwe Baraka Mohamed shamte amesema Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Huseein Ali Mwinyi atashinda vita ya kupigania maendeleo na kujenga uchumi imara.
Pia amemtaja kiongozi huyo amezitumia vyema siku mia moja huku serikali yake ikisaini mikataba mikubwa ya kiuchumi . Hayo yameelezwa na Mwanasiasa huyo mashuhuri akimtaja Rais Dkt Mwinyi ni kiongozi kijana ,mwenye fikra mpya aliyejengea matumaini chanya
Shamte amesema tokea wakati wa kampeni amekuwa akisema amejitolea kwa dhati yake kuivusha nchi na watu wote na hataongoza kwa upendeleo wowote.
Amesema kazi ya kuleta mabadiliko ni kama mapambano vitani hivyo Dkt Mwinyi ataibuka mshindi kwenye uwanja wa mapambano hayo
Shamte amesema amejenga matumaini kwa kutimiza ahadi zake na kuwa kiungo katika jamii na kukusanya kwa bilioni 4 mwezi Disemba mwaka uliopita kwa tofauti ya bilioni mbili zilizokuwa zikikusanywa kwa mwaka ni mafanikio makubwa.
Aidha amesifu hatua za kuanzishwa kwa mahakama ya udhalilishaji akisema vitendo viovu vilikithiri na sasa imepatilkana tiba yake na kumpongeza kwa kuendeleza maridhiano ya kisiasa, kudumisha umoja, amani na mshikamano wa kitaifa.
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *