SERIKALI INAFANYA JITIHADA ZA KUBORESHA UENDELEZWAJI WA VIWANDA VYA NGUO NCHINI.

SERIKALI INAFANYA JITIHADA ZA KUBORESHA UENDELEZWAJI WA VIWANDA VYA NGUO NCHINI.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na wadau wa sekta ya nguo na mavazi ili kusikiliza changamoto wanazokutana nazo na mapendekezo yao katika kuboresha na kukuza sekta hiyo. Akizungumza na wadau hao katika kikao kilichofanyika Februari 9,2021 katika ukumbi wa Chuo cha Biashara (CBE ) jijini Dodoma

Inaweza kuwa picha ya Watu 2, watu wanakaa, watu wanasimama na ndani
Inaweza kuwa picha ya Watu 6, watu wanakaa, watu wanasimama na ndani
Inaweza kuwa picha ya Watu 4, watu wanakaa na ndani

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na wadau wa sekta ya nguo na mavazi ili kusikiliza changamoto wanazokutana nazo na mapendekezo yao katika kuboresha na kukuza sekta hiyo.

Akizungumza na wadau hao katika kikao kilichofanyika Februari 9,2021 katika ukumbi wa Chuo cha Biashara (CBE ) jijini Dodoma Mhe Naibu Waziri amewaomba kuwasilisha changamoto walizonazo na rasmi za mipango mikakati ya kuboresha na kuendeleza Viwanda na Biashara katika sekta hiyo ili kukuza uchumi wa nchi.

Aidha katika kikao hicho kilichojumuisha wadau ambao ni watengenezaji na waagizaji wa nguo na mavazi kutoka nje ya nchi, wadau hao waliwasilisha changamoto na mapendekezo yao kwa Mhe. Naibu Waziri wakiwa na lengo la kuboresha na kukuza sekta hiyo.

Tanzania inaviwanda 11 vya nguo na mavazi vinavyofanya kazi kwa sasa na vinatoa ajira ya moja kwa moja ya jumla ya wafanyakazi takribani 15300 na zisizo za moja kwa moja takribani 45000.

Aidha, Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali katika kuendeleza sekta ya nguo na mavazi nchini ikiwemo kukuza soko la ndani la bidhaa hizo pamoja na kuandaa na kutekeleza Mkakati wa kuendeleza Sekta ya pamba nguo hadi mavazi ( Cotton to Clothing Strategy C2C 2016 – 2020 ) na kuuhuisha ambapo utekelezaji wake utaanza mwaka 2021 – 2032.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »