SI KILA BAYA UNALOTENDWA NI SHETANI

SI KILA BAYA UNALOTENDWA NI SHETANI

Bwana Yesu Kristo asifiwe Wana wa Mungu aliyehai ❗ Ni siku nyingine Tena Mungu ameachilia neema yake kwetu tu wazima na wenye pumzi. Leo Mungu anasema na kanisa lake ili uvuke ulipo kwama lakini pia upate Amani ndani ya moyo wako katikati ya mapito yako. Haijalishi Ni Nani anaye/aliyekutenda lakini Jambo la msingi ujue si

Bwana Yesu Kristo asifiwe Wana wa Mungu aliyehai ❗ Ni siku nyingine Tena Mungu ameachilia neema yake kwetu tu wazima na wenye pumzi. Leo Mungu anasema na kanisa lake ili uvuke ulipo kwama lakini pia upate Amani ndani ya moyo wako katikati ya mapito yako. Haijalishi Ni Nani anaye/aliyekutenda lakini Jambo la msingi ujue si kila akutendaye ubaya ni Yeye wakati mwingine Ni Mungu mwenyewe anaachilia ubaya ili akutoe ulipo na kukupeleka mahali pengine pakubwa zaidi , pa mafanikio zaidi, akupandishe ngazi ili ukue hekima ya namna ya kuenenda utakapofika pale juu. Haya tunayaona kwa Mtoto wa Yakobo , Yusufu Kama ilivyoandikwa;

Mwanzo 45:4-8

4 Yusufu akawaambia ndugu zake, Karibuni kwangu; basi, wakakaribia. Akasema, Mimi ni Yusufu, ndugu yenu, ambaye mliniuza kwenda Misri.

5 Basi sasa, msihuzunike, wala msiudhike nafsi zenu, kwa kuniuza huku; maana Mungu alinipeleka mbele yenu kuhifadhi maisha ya watu.

6 Maana miaka hii miwili njaa imekuwa katika nchi, na iko tena miaka mitano isiyo na kulima wala kuvuna.

7 Mungu alinipeleka mbele yenu kuwahifadhia masazo katika nchi, na kuwaokoa ninyi kwa wokovu mkuu.

8 Basi si ninyi mlionipeleka huku, ila Mungu; naye ameniweka kama baba kwa Farao, na bwana katika nyumba yake yote, na mtawala katika nchi yote ya Misri.

Sikiliza mpendwa wangu , Naomba Mungu akupe neema ya kujua sababu ya kutokea mabaya . Elewa kwamba SI yote ya Shetani mengine Ni mpango wa Mungu aliyehai. Ndo maana unaona Yusufu namna ambavyo anawambia ndugu zake ,SI kwmaba alijua Ila Sasa ndo ameelewa kwanini hakuuwawa na kwanini aliuzwa huko Misri . Hii Ni Siri ya ajabu Sana kwa Wateule wengi kuijua. Badala ya kumchukia anapambana nawe usku na mchana mpende maana Mungu anaelewa Vita yako lkn anataka uvuke mahali penye mafanikio na ushuhuda mkuu wa Mungu aliyehai.

Sikiliza, hata Kama si mpango wa Mungu hayo mapito ,elewa tu shida siyo mwili huo inaonekana kwa macho ya nyama yaani si mtu unayemuona Bali Ni Roho ya adui ambayo imepandwa ndani yake. Hiyo ndiyo inatakiwa ishughulikiwe. Na hata katika hili elewa na Mungu anakusudi kwako la kukutaka kukomaza kiroho na kukuvusha hatua fulani.

Mungu akubariki Sana kwa kupokea ,Damu ya Yesu Kristo aliyehai inene mema kwaajili kukua kwetu kiroho .

Have a blessed day

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »