Kamonga: Wafugaji na Wakulima wamekuwa na tabia ya kuhama hama.

Kamonga: Wafugaji na Wakulima wamekuwa na tabia ya kuhama hama.

Na Barnabas kisengi Mpwapwa February 10  2021 Tatizo la shule za msingi za mikondo zinazoanzishwa ujenzi na wananchi katika wilaya ya mpwapwa mkoani Dodoma kwa kutoendelea na ujenzi wa vyumba vingine vya madarasa limekuwa sugu hasa katika shule hizo ambazo zinakuwa zimesajiliwa na kuipelekea serikali mzigo mkubwa wa kuendelea na ujenzi wavyumba vya madarasa katika shule

Na Barnabas kisengi Mpwapwa February 10  2021


Tatizo la shule za msingi za mikondo zinazoanzishwa ujenzi na wananchi katika wilaya ya mpwapwa mkoani Dodoma kwa kutoendelea na ujenzi wa vyumba vingine vya madarasa limekuwa sugu hasa katika shule hizo ambazo zinakuwa zimesajiliwa na kuipelekea serikali mzigo mkubwa wa kuendelea na ujenzi wavyumba vya madarasa katika shule hizo


Kauli hiyo imebainishwa na mdhibiti ubora mkuu wa wilaya ya mpwapwa mwalimu Grece kamonga alipoitembelea na kuikagua shule ya msingi makulu iliyopo Kata ya berege wilayani mpwapwa na kujionea hali halisi ya uwepo wa vyumba Vinne vya madarasa vilivyo jengwa muda mrefu zaidi ya miaka 4 lakini hadi sasa hawajavikamilisha na bado Kuna wanafunzi wengine wamekuwa wakisomea nje ya madarasa kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa

“Tatizo kubwa ni wananchi wetu wafugaji na wakulima wamekuwa na tabia ya kuhama hama maeneo na Huku wakiwa wanaendelea kuzaliana na kutafuta maeneo ya malisho sasa unakuta Kuna vitongiji vinaanzishwa maeneo mengi na wanakuwa mbali na maeneo yaliyotengwa kwa huduma za jamii Kama elimu,afya na huduma nyingine unakuta watoto wanakua mbali na shule hivyo inawalazimu kuanzisha shule ya mkondo kwa wale watoto wadogo wadarasa la Kwanza,pili na latatu na hapo shule  inakuwa imesajiliwa na mtoto anapoingia darasa la nne anatakiwa akasome shule mama wazazi utaona wanakataa kuwapeleka huko kwa kuwa wanaona shule imesajiliwa hawakumbu kuwa walianzisha ujenzi wa vyumba vichache vya madarasa hivyo kuwafanya wanafunzi wasomee nje  Kama shule hii ya makulu wanafunzi wamekuwa wakisomea nje kwa muda mrefu jambo ambalo linashusha kiwango cha ufaulu”amesema grace kamonga


Mwalimu kamonga amesema kuwa  wazazi wasiipe serikali mzigo mzito usio na sabababu Kama wanaamua kujenga shule wanafahamu taratibu kupita mikutano ya vitongoji vijiji na Kata husika hii itawasaidia kuweza kuanzisha shule na serikali kuwaunga mkono hasa kwa serikali hii ya awamu ya tano inaunga sana jitihada za elimu,afya na miundombinu hivyo wanapo taka kuanzisha ujenzi wa vyumba vya madarasa wafuate taratibu na sharia 

“shule hii ya msingi makulu imejengwa muda mrefu sasa wazazi nawaomba waendelee na jitihada za kuanza kujenga misingi mingine ya madarasa matatu na kuinua maboma ili Waweza kutimiza ndoto yao ya kuwa na vyumba Saba vya madarasa na wakianzisha hiyo misingi na maboma serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Magufuli itawaunga mkono jitihada hizo ili kuweza kuikamilisha shule hii ambayo tayari umekwisha sajiliwa hivyo wakiikamilisha watapewa huduma zote zinazostahili zinazotolewa na serikali Kama kuongezewa walimu na huduma nyingine nyingi za elimu”amesema mzibiti ubora mkuu wa wilaya ya mpwapwa mwalimu Grece kamonga


Pia mwalimu kamonga amewataka walimu,wanafunzi na wazazi kila moja kutimiza wajibu wake katika eneo lake huku akiwataka walimu wakuu kuhakikisha wanapanga ratiba za vipindi za walimu na kuzibandika katika ofisi zao ili kila mwalimu ajue anavipindi vingapi pindi anapo kuwepo kazini na itasaidia kujua mwalimu gani hajaingia darasani kwa sababu gani na itasaidia kuwafahamu walimu watoro na wavivu pindi wao wanapopita kukagua shule wilayani hapo

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »