Yaliyojiri wakati Rais John Magufuli akizindua Soko kuu mkoani Morogoro lijulikanolo kwa jina la Soko la Chifu Kingalu

Yaliyojiri wakati Rais John Magufuli akizindua Soko kuu mkoani Morogoro lijulikanolo kwa jina la Soko la Chifu Kingalu

Aliyoyasema Rais wa Jamhuri ya Muungan wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Nimefurahi sana kufika Morogoro, nawashukuru kwa ushujaa mkubwa mlioufanya Morogoro. Ilikuwa nipitilize lakini leo nalala hapa ili nijue matatizo yote ya hapa Morogoro.Soko Kuu la Morogoro ni sehemu ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa masoko 22, stendi za mabasi, stendi za malori,

Aliyoyasema Rais wa Jamhuri ya Muungan wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli


Nimefurahi sana kufika Morogoro, nawashukuru kwa ushujaa mkubwa mlioufanya Morogoro. Ilikuwa nipitilize lakini leo nalala hapa ili nijue matatizo yote ya hapa Morogoro.
Soko Kuu la Morogoro ni sehemu ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa masoko 22, stendi za mabasi, stendi za malori, na machinjio yanayojengwa nchi nzima kwa gharama ya shilingi Bilioni 361.033. Serikali imetoa asilimia kubwa ya fedha hizi na hadi sasa masoko 9 yamekamilika ikiwemo hili la Morogoro.


Uwepo wa masoko una manufaa mengi kwa maendeleo. Wakulima na wafanyabiashara wanapata maeneo mahususi ya kuuza bidhaa zao lakini pia wananchi wanapata maeneo ya huduma na Serikali itaweza kukusanya kodi katika maeneo hayo.


Nimeambiwa wafanyabiashara zaidi ya 2500 wanafaidika na soko hili. Nimepata maelezo mazuri wakati nimefika kwenye soko hili na nimesikia kero za wafanyabiashara ndani ya soko hili.

Mwananchi akibeba mzigo wake usiozidi tani moja, hatakiwi kutozwa tozo yoyote. Huu ndio utaratibu nchi nzima. Hii ndio sheria ninayoifahamu na hii ndio sheria ninayoilinda.
Kwenye soko hili wapo waliopewa vizimba vyao bila tatizo lakini wapo waliopewa kwa kukodishwa na madalali na baadhi ya madalali hao ni wafanyakazi wa manispaa. Nimepata Ushahidi wa mtu mmoja, badala ya kulipa TSH 20,000/- analipa TSH 50,000/- na anatozwa na mfanyakazi wa manispaa.


Nimetoa maelekezo kwa wafanyakazi wa manispaa ya Morogoro. Wafanyakazi warudishe fedha zote walizochukua kwa kukodisha vizimba. Hili soko limejengwa kwa fedha za Serikali. Waziri TAMISEMI simamia hili. Wale wote waliochukua hela na kula faida wakati hili jengo ni mali ya Serikali warudishe hizo hela, hiyo ndio njia nzuri ya kuwasamehe. Ole wake atakayekiuka agizo hili.


Morogoro ina historia yake na mimi napenda siku zote tuwe tunaikumbuka historia yake. Hapa Morogoro pamewahi kuwa na Chifu na nafikiri bado yupo, Chifu wa Kabila la Waluguru anaitwa Kingalu. Kwa mamlaka niliyopewa, naliita soko hili ‘Soko la Chifu Kingalu’ , hii ni kwa heshima ya chifu Kingalu ambaye ana mchango mkubwa hapa Morogoro.

Aliyoyasema Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Joseph Nyamhanga


Soko Kuu la Morogoro ni miongoni mwa masoko 22 yaliyojengwa katika maeneo mbalimbali nchini ambayo yamegharimu shilingi Bilioni 120, mengi yameanza kutumika na mengine yapo katika hatua mbalimbali za ujenzi 

Historia ya Soko Kuu la Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro inarudi mpaka mwaka 1953 lilipojengwa soko kwa mara ya kwanza, miundombinu ilikuwa imechakaa na kuharibika sana hivyo kushindwa kukidhi mahitaji ya watumiaji ukilinganisha na ukuaji wa Manispaa ya Morogoro.


Ujenzi wa soko hili la kimkakati ulianza Juni 20, 2018 na kukamilika Julai 20, 2020. Ujenzi umegharimu shilingi Bilioni 17.656 zinazojumuisha shilingi Bilioni 14.962 kwa ajili ya ujenzi wenyewe na shilingi Bilioni 2.693 ambazo ni malipo ya ongezeko la thamani.

Aliyoyasema Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Loata Sanare


Mhe. Rais tumehangaika na maswala ya afya, ulitupatia fedha za kujenga hospitali vijijini, katika Wilaya zote hospitali zinafanya kazi na tumejenga vituo vya afya 17 kwa fedha ulizotupatia.

Mwaka huu vijana wengi wamefaulu, tumekuwa na kazi ya kujenga madarasa 267 na tumefikia asilimia 87%, wengi wameshaanza shule, tutahakikisha waliobaki wanaingia shule pia – Loata Sanare, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

Imeandaliwa na idara ya Habari MAELEZO

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »