Serikali yaanza kutumia Ndege kudhibiti nzige Wilayani Loliondo

Serikali yaanza kutumia Ndege kudhibiti nzige Wilayani Loliondo

Na Barnabas kisengi loliondoFebruary  21 2021 Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda leo ametembelea eneo la Longido ambayo yamevamiwa na nzige  na kuwa kuanzia kesho ndege maalum itafanya kazi kupulizia viuatilifu kuua nzige hao. Prof. Mkenda amesema wananchi wasiwe na hofu nzige wote watadhibitiwa kupitia wataalam wa Wizara ya Kilimo waliopo kwenye maeneo yote yenye

Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda

Na Barnabas kisengi loliondoFebruary  21 2021


Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda leo ametembelea eneo la Longido ambayo yamevamiwa na nzige  na kuwa kuanzia kesho ndege maalum itafanya kazi kupulizia viuatilifu kuua nzige hao.

Prof. Mkenda amesema wananchi wasiwe na hofu nzige wote watadhibitiwa kupitia wataalam wa Wizara ya Kilimo waliopo kwenye maeneo yote yenye dalili za uwepo wa wadudu hao.


“Kuanzia kesho (22.02.2021)  ndege maalum itaanza kazi kupulizia sumu kuua nzige waliovamia maeneo ya Longido na Simanjiro” amesema Waziri Mkenda


Waziri Mkenda amesema tayari wataalam wa Taasisi ya Utafiti wa viuatilifu vya  kudhibiti visumbufu (TPRI) wapo wilayani Longido na Simanjiro wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wake Dkt. Efrem Njau .

Aidha ametoa wito kwa wananchi kutookota wala kula nzige watakaokuwa wameuawawa na viuatilifu(sumu) kwenye maeneo yote ambapo ndege itapita kuua nzige.


Pili,ameagiza wataalam na Watendaji wa vijiji na Kata kutoa taarifa Kwa wananchi juu ya uwepo wa kazi ya kuua nzige hivyo wasiwe na hofu.
“Wananchi wakiona nzige wameanguka chini wamekufa wasiwachukue au Kula kwa kuwa wengi watakuwa wamekufa Kwa sumu” alisisitiza Prof. Mkenda


Waziri huyo wa kilimo amesisitiza kuwa serikali itahakikisha mazo ya wakulima na malisho ya Mifugo hayaribiwi na nzige ndio maana ametembelea eneo hili la Longido ambapo amebainisha mafanikio ya kuwadhibiti tangu walipoingia nchini mwezi Januari mwaka huu kwenye baadhi ya maeneo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido Jumaa Mhina ametoa agizo shule zote za msingi na sekondari kwenye maeneo ambapo ndege itapuliza viuatilifu kusitisha masomo Kwa muda wa siku 4 kuanzia kesho ili kudhidhibi watoto wasije wakapata madhara endapo watashika au kuchezea nzige watakaokufa.


Anaye Mbunge wa Longido Dkt. Steven Lemomo Kiruswa ameiomba serikali iharakishe kupulizia viuatilifu ili nzige wasije leta madhara kwa mifugo na wakulima kwenye maeneo ya Longido .

” Leo ni siku ya tatu nzige wameingia Longido, tunaomba jitihada za wataalam wa TPRI kuwadhibiti ili wasilete madhara kwetu sisi wafugaji tunaotegemea nyasi kwa malisho” amesema Mbunge Kiruswa.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »