LIGI KUU TANZANIA BARA KUPIGWA TENA LEO

Ligi kuu tanzania bara inatarajia kuendelea leo kwa michezo miwili itakayopigwa katika viwanja viwili tofauti Waoka mikate wa jiji la Dar es salaam Azam fc wanataraji kuingia uwanjani kumenyana dhidi ya wajelajela Tanzania Prisons, mchezo ambao utapigwa katika uwanja wa Azam Complex Chamazi nje kidogo na jiji hilo mechi itaanza majira ya saa moja usiku

Ligi kuu tanzania bara inatarajia kuendelea leo kwa michezo miwili itakayopigwa katika viwanja viwili tofauti

Waoka mikate wa jiji la Dar es salaam Azam fc wanataraji kuingia uwanjani kumenyana dhidi ya wajelajela Tanzania Prisons, mchezo ambao utapigwa katika uwanja wa Azam Complex Chamazi nje kidogo na jiji hilo mechi itaanza majira ya saa moja usiku

Azam Fc wanaingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kupata ushidi mnono wa magoli 2 – 1 walioupata katika uwanja wao huo wakati wakipepetana dhidi ya Mbeya City.

Ikiwa Azam FC ipo nafasi ya tatu na pointi 36 baada ya kucheza mechi 20 inakutana na Prisons iliyo nafasi ya 8 na pointi zake 25.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela,  Azam FC ilishinda bao 1-0 lililopachikwa na Prince Dube hivyo leo kazi itakuwa moja kwa Azam FC kulinda rekodi yao huku Prisons wakiwa na hesabu za kutibua hesabu za Azam FC.

Mchezo mwingine utakuwa ni kati ya Dodoma Jiji dhidi ya Polisi Tanzania mechi hii itapigwa katika uwanja wa jamhuri mkoani Dodoma majira ya saa kumi kamili jioni

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »