Wakazi zaidi ya elfu 3000 Kata ya kilimani Wako hatarini kutokana na Ubovu wa miundombinu ya barabara.

Wakazi zaidi ya elfu 3000 Kata ya kilimani Wako hatarini kutokana na Ubovu wa miundombinu ya barabara.

Na Barnabas kisengi Dodoma February  22  2021 Wakazi zaidi ya elfu 3000 wa mtaa wa chinyoya Kata ya kilimani jijini Dodoma wako hatarini kubaki kuwa kisiwa kutokana na kuharibika vibaya kwa barabara za mtaa huo jambo ambalo hupelekea kushindwa kupitika kwa magari na hata watembea kwa miguu huku wakiwa na wagonjwa kunawapa adha kubwa ya kuweza

Na Barnabas kisengi Dodoma February  22  2021


Wakazi zaidi ya elfu 3000 wa mtaa wa chinyoya Kata ya kilimani jijini Dodoma wako hatarini kubaki kuwa kisiwa kutokana na kuharibika vibaya kwa barabara za mtaa huo jambo ambalo hupelekea kushindwa kupitika kwa magari na hata watembea kwa miguu huku wakiwa na wagonjwa kunawapa adha kubwa ya kuweza kuwafuata katika maeneo yao wanayoishi na kuwasababishia kuonekana Kama wanaishi kisiwani kwa kuharibika miundombinu ya barabara hizo za mtaa huo wa chinyoya 

Wakizungumza na kituo hichi kwa niaba ya wenzao mussa mkunda na mbamba uswege (mstaafu) wameiomba serikali kupitia wakala wake wa barabara za mijini na vijijini Tarula  kuweza kurekebisha miundombinu ya mtaa huu kabla ya maendeleo kuharibika na kuwafanya Wawe Kama wanaishi kisiwani kwa uharibifu mkubwa wa barabara hizo za mtaa wao


“hapa tunaiomba serikali itusaidie kurekebisha hizi barabara za mtaa maana tunazitumia zaidi ya wakazi Kama elfu 3000 sasa kama unamgonjwa hapa mtaani ni shida jinsi ya juu kuingia na gari kumpakia na hata wafanya biashara nao ni kazi kuleta gari kwa ajili ya kushusha mzigo maana magari hayaingii kabisa hapa mtaani na hata wenye magari yao binafsi wamekuwa wakishindwa kurudi nayo na kuyaacha upande wa pili wa mtaa mwingine kwakweli hii ni adha kubwa tunayoipata hata kwa swala la kiuchumi linakuwa likishuka hapa mtaani kwa kushindwa kufanya biashara kutokana na uharibifu huu mkubwa wa miundombinu ya barabara”amesema mbamba uswegwe (mstaafu) 

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa huo wa chinyoya Bi Faustina Bendera amekiri kuwapo kwa changamoto hiyo kubwa ya kuharibika kwa miundombinu ya barabara zote za ndani za mtaa wake jambo ambalo limefanya mtaa mzima kutopitika kwa vyombo vya usafiri Kama magari 
“Ni kweli mtaa wangu kwa sasa haupitiki kabisa kwa magari yani imekuwa ni kero kubwa kwa wananchi wangu yani hapa ukiwa na mgonjwa lazima mmubebe hadi barabarani huko chini mtaa mwingine ndio apakiwe kwenye gari na kukimbizwa hospital na hata wafanya biashara nao wanashindewa kuleta bidha zao kutokana na kushindwa kupitika kwa barabara ya mtaa jambo ambalo hupelekea kushuka kwa uchumi katika mtaa wangu kwa sasa”amesema Faustina Bendera


Aidha Faustina amesema tayari swala hilo alisha lifikisha kwenye vikao vya juu vya Kata na alimshirikisha Diwali pomoja na mbunge wa Jimbo la Dodoma Mh Antony mavunde juu ya barabara hizo za mtaa amazo zote zimeharibika vibaya

“Nilivyoona hali hii kwakuwa mimi ni mwenyekiti wa mtaa nilimshirikisha mbunge na diwani wangu wa Kata na tunashukuru mbunge tulipo mwambia tu alifika kwa wakati na kujionea hali ya uharibifu mkubwa wa miundombinu hiyo ya barabara na kutuahidi atalishulikia kwa haraka sana kwa kuwashirikisha wakala wa barabara za mijini na vijijini Tarula ili kuokoa hali hii ambayo inajionyesha”amesema faustina


Diwani wa Kata hiyo ya kilimani Mh Neema mwaluko amesema atahakikisha kwa kushirikiana na mbunge watajitahidi walau warejebishe barabara chache zianze kupitika wakati wakisubiri mvua zikatike ili waanze mpango wa kutengeneza barabara hizo za mtaa kwani mtaa huo ndio umefanyiwa maboresho ya upimaji wa mtaa hivyo barabara za mitaa zilikuwa bado hazijaanzwa kutengenezwa kwa kiwango kizuri

Mtaa huo wa chinyoya ni mtaa ambao tako uhuru mtaa huu ulikuwa haujapimwa wananchi walikuwa wakiishi kienyeji tu ila kwa sasa kwa kupita mwenyekiti wa mtaa huu bi Faustina Bendera kwa kushirikiana na diwani na mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini na serikali ya awamu ya tano tayari wamefanikisha jambo la kufanyiwa maboresho ya upimaji wa aridhi wa mtaa huo ambapo sasa wananchi wamekuwa wakiishi kwa amani sasa baada ya kupimiwa viwanja vyao na kupewa hati miliki.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »