Maadhimisho siku ya Wanawake duniani yatafanyika katika ngazi za mikoa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kila mkoa husika

Maadhimisho siku ya Wanawake duniani yatafanyika katika ngazi za mikoa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kila mkoa husika

Na Barnabas kisengi Dodoma February 23 2021 Tanzania ni miongini mwa nchi mwanachama za umoja wa mataifa ambazo kila ifikapo March 8 kila mwaka huadhimisha siku ya wanawake duniani ambapo maadhimisho haya yalianza mwaka 1911 kufuatia wanawake wafanyakazi katika sekta ya viwanda nchini marekani waliokuwa wakipinga mazingira duni ya kazi na vitendo vya unyanyasaji katika ajira

Na Barnabas kisengi Dodoma February 23 2021


Tanzania ni miongini mwa nchi mwanachama za umoja wa mataifa ambazo kila ifikapo March 8 kila mwaka huadhimisha siku ya wanawake duniani ambapo maadhimisho haya yalianza mwaka 1911 kufuatia wanawake wafanyakazi katika sekta ya viwanda nchini marekani waliokuwa wakipinga mazingira duni ya kazi na vitendo vya unyanyasaji katika ajira ikiwemo kulipwa mshahara mdogo kwa kazi

Waziri wa Afya,maendeleo ya Jamii,jinsia,wazee na watoto Dkt Dorothy Gwajima amesema mnamo mwaka 1945 umoja wa nchi wanachama ulipitisha azimio la nchi wanachama kuadhimisha siku hii ambayo nchi ya Tanzania ilianza kuadhimisha siku hii kitaifa kuanzia mwaka 1997 na mnamo mwaka 2005 serikali ilielekeza maadhimisho haya yafanyike kila baada ya miaka mitano ili kutoa fursa kwa uwezeshaji kwa kuzingatia tamko hilo serikali ilitekeleza kuwa katika miaka nyingine maadhimisho haya yafanyike kimkoa ambapo kila mkoa utaandaa taratibu wake kulingana na mazindira yao


Aidha waziri Dkt Gwajima amesema mwaka 2020 maadhimisho haya yalifanyika kitaifa mkoani simuyu lakini kwa mwaka 2021 maadhimisho haya ya siku ya wanawake duniani yatafanyika katika ngazi za mikoa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kila mkoa husika


Dkt Gwajima ametoa rai kwa mikoa kuendelea na uratibu wa maadhimisho haya kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali katika maeneo yao na kwa upande wa wadau watakao shiriki maadhimisho haya wawasiliane na ofisi za makatibu tawala wa mikoa na pindi watakapo itaji ushiriki wa wizara wao wako tayari muda wote ili kufanikisha sikukuu hii ya wanawake duniani yenye kauli mbiu isemayo.
“WANAWAKE KATIKA UONGOZI CHACHU KUFIKIA DUNIA YENYE USAWA”

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »