RC ATOA MWEZI MMOJA KUJENGWA VYUMBA VITANO VYA MADARASA SEKONDARI YA SUA MOROGORO

RC ATOA MWEZI MMOJA KUJENGWA VYUMBA VITANO VYA MADARASA SEKONDARI YA SUA MOROGORO

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare ametoa mwezi mmoja kwa watendaji wa kata mbili za Mbuyuni na Magadu manispaa ya Morogoro kuhakikisha wanajenga vyumba 5 vya madarasa katika shule ya sekondari SUA ili kumaliza mgogoro uliodumu kwa muda refu katika kata hizo kwa kila mmoja kudai shule hiyo ipo upande wake Uamuzi huo

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare ametoa mwezi mmoja kwa watendaji wa kata mbili za Mbuyuni na Magadu manispaa ya Morogoro kuhakikisha wanajenga vyumba 5 vya madarasa katika shule ya sekondari SUA ili kumaliza mgogoro uliodumu kwa muda refu katika kata hizo kwa kila mmoja kudai shule hiyo ipo upande wake

Uamuzi huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro alipotembelea Kata hizo za na kukuta hakuna dalili yoyote ya ujenzi wa vyumba vya madarasa sababu kubwa ikiwa ni mvutano uliopo wa nani mmiliki halali wa shule ya Sekondari ya SUA.

Baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote mbili mkuu wa mkoa akatoa maelekezo kuwa mvutano huo hauna tija kwa wananfunzi wanaohitaji kuingia madarasa.

Aliwataka watendaji hao kujenga vyumba hivyo pembeni kidogo mwa majengo ya shule hiyo ya SUA lakini ndani ya eneo la shule hiyo ili kukamilisha haraka na hivyo kukabiliana na changamoto ya upungufu wa madarasa katika shule hiyo.

“Kata ya Mbuyuni ina mitaa sita itajenga vyumba viwili vya madarasa na kata ya Magadu yenye mitaa tisa itajenga vyumba vitatu vya madarasa na nawapa mwezi mmoja watendaji kukamilisha ujenzi huu ufike usawa wa linta kisha mumkabidhi mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa yeye ataalizia” alisema Sanare.

Kadharika Sanare aeshauri kuwa  mara baada ya kukailika kwa majengo hayo ndipo viongozi wanaweza kukaaa siku zijazo abampo kupitia majengo hayo wanaweza kuamua kuifanya shule inayojitegemea, hivyo kila kata kuwa na shule yake na kuondoa mvutano uliokuwepo wa kutaka kila mmoja kuwa mmiliki wa shule hiyo.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Mbuyuni Mhe. Samwel Msuya amebainisha changamoto iliyokuwepo katika ujenzi wa Shule ya Sekondari ya SUA kuwa ni baada ya kata yake ya Mbuyuni kushtakiwa na kukatazwa kuendeleza shule hiyo hali ambayo ilipelekea kudolora kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Msuya amesema hadi sasa changamoto hiyo imekwishatatuliwa na wananchi wa mbuyuni na magadu wapo tayari kuendeleza ujenzi wa madarasa katika Shule hiyo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »