“makambi shuleni si suluisho la ubora wa Elimu”Katibu mkuu TAMISEMI Gerald Mweli.

“makambi shuleni si suluisho la ubora wa  Elimu”Katibu mkuu TAMISEMI Gerald Mweli.

Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa(TAMISEMI)Bw. Gerald Mweli amewataka walimu kuwekeza katika ufundishaji  kwani Makambi shuleni sio suluhisho la kiwango bora cha Elimu Nchini naTayari Barua Rasmi ya kukataza makambi mashuleni tayari imeshatolewa. Mweli Ameyasema hayo katika kikao cha wadau wa Elimu Wilayani kongwa mkoani Dodoma baada ya


Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa(TAMISEMI)Bw. Gerald Mweli amewataka walimu kuwekeza katika ufundishaji  kwani Makambi shuleni sio suluhisho la kiwango bora cha Elimu Nchini naTayari Barua Rasmi ya kukataza makambi mashuleni tayari imeshatolewa.


Mweli Ameyasema hayo katika kikao cha wadau wa Elimu Wilayani kongwa mkoani Dodoma baada ya wadau hao kuelezea changamoto mbalimbali zinazokwamisha kiwango bora cha ufaulu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

Mweli Amesema Kuweka Makambi mashuleni kwa miezi mitatu hakujengi ufahamu wa wanafunzi bali ni kukimbia Tatizo la kuwajengea uwezo wanafunzi kifikra na kushughulika na upandaji wa alama za ufaulu jambo ambalo linapelekea kufeli kwa wanafunzi wengi wafikapo hatua za juu.


Kikao hicho kilichowezeshwa na Orex Gas na Maziwa ya Asasi kilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa Elimu akiwemo Spika wa Bunge La Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Elimu wakiwemo Walimu wakuu,viongozi wa serikali za mitaa,madiwani, watendaji wa Kata na vijiji kilijadili.

Kadhalika Amesema kuwa lengo la mitihani ya kidato cha pili ni kusadia kuwapanga wanafunzi katika masomo wanayoweza kuyahimili wakiingia kidato cha tatu kulingana na uwezo wao kiakili,alishauri kila mwanafunzi wa kidato cha tatu awe na Taarifa zake sahihi za mwenendo wa kitaaluma kutoka kidato cha kwanza.


“Hivyo Tukitumia vizuri mitihani ya kidato cha pili Tutatapa wataalam walio Bora zaidi Nchini”alisisitiza mweli
Kufuatia ombi la Spika wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Joab Ndugai ambaye ndiye mbunge wa jimbo la Kongwa la shule za kutwa za kidato cha tano na sita ili kusaidia wazazi wenye uchumi mdogo kumudu kusomesha watoto Bw. Mweli alisema Sera ya Elimu inaruhusu kuwa na shule  hizo hivyo wasisite kuzianzisha endapo mazingira yanaruhusu.


Afisa Elimu sekondari Bw.ABduli Nyambi Aliezea Baadhi ya changamoto za ufaulu duni ni pamoja na Uhaba wa walimu wa Sayansi na Hisabati,ukosefu wa fedha za kuendeshea mitihani ya majaribio,utoro wa wanafunzi,upungufu wa samani na vyumba vya madarasa ,utendaji usioridhisha kwa Baadhi ya watendaji na maafisa Elimu Kata,wakuu wa shule na walimu, pamoja na Jamii kutotambua umuhimu wa Elimu. 

Mwenyekiti wa CCM Wilayani kongwa Mwl Abdi akitoa maoni yake amesema iko haja ya kila Mkuu wa shule kuwa na Taarifa za ufundishaji wa vipindi vya masomo kwa kuweka daftari maalumu la kusaini kila kipindi kwa walimu ili iwasaidie katika tathmini ya ufundishaji na kiwango cha elimu bora.

Naye Bi Jema kihwelu Mkuu wa shule ya Sekondari Kibaigwa alisema Tafsiri ya utoro isiishie kwa wanafunzi kutofika shule bali ihesabu Utoro wa vipindi vya masomo kwa wanafunzi ili kuboresha ubora wa Elimu.

Katika kikao hicho naibu katibu Mkuu alipata fursa ya kuzindua mpango mkakati wa kuboresha Elimu pamoja na kutoa zawadi kwa shule zilizofanya vizuri na zilizofanya vibaya kupewa vyeti vya himizo.

Na Barnabas kisengi kongwa.

February  26 2021

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »