JKT na wizara ya kilimo zatia saini ya mkataba wa maridhiano katika kuinua kilimo hapa nchini Tanzania

JKT na wizara ya kilimo zatia saini ya mkataba wa maridhiano katika kuinua kilimo hapa nchini Tanzania

Na saleh Ramadhani Dodoma February  26 2021 JESHI la kujenga Taifa (JKT)  limetia saini mkataba wa maridhiano na Wizara ya Kilimo  kwa kutambua kuwa kilimo ndiyo uti wa mgongo. Hayo yamebainisha leo Jijini hapa na Mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa JKT Meja Generali Charles Mbuge amesema mashirikiano hayo yataleta tija katika uzalishaji mzuri wa sekta

Na saleh Ramadhani Dodoma February  26 2021


JESHI la kujenga Taifa (JKT)  limetia saini mkataba wa maridhiano na Wizara ya Kilimo  kwa kutambua kuwa kilimo ndiyo uti wa mgongo.

Hayo yamebainisha leo Jijini hapa na Mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa JKT Meja Generali Charles Mbuge amesema mashirikiano hayo yataleta tija katika uzalishaji mzuri wa sekta ya kilimo kwani Taifa likiwa na njaa  shughuli za kiuchumi haziwezi kufanyika.

Aidha Meja Generali Mbuge amesema kilimo ndio uti wa mgongo ambapo kwa Tanzania Kilimo kinahusisha matabaka yote  wenye kipato na wasio na kipato

“Makubaliano hayo Kati yaJeshi la kujenga Taifa (JKT) yamekuja wakati muafaka kwani vijana wengi wa Tanzania wamekua wakijitolea  kwenye mafunzo hivyo wakiwa ndani ya JKT watapatiwa mafunzo ya Kilimo ambapo na wakimaliza mafunzo yao na kurudi katika maeneo yao walipotoka wakawe mfano mzuri katika sekta ya kilimo.

Pia ameongeza kuwa “Jeshi ni chombo pekee ndani ya Taifa letu hivyo endapo likitumiwa vizuri litaleta manufaa makubwa katika Taifa”amesema 

Hata hivyo amesema JKT imeshaanza shughuli za Kilimo kwa mazao ya kimkakati Katika maeneo mbalimbali ya hapa Nchini.


Naye Kanali Hassan Mabena ambae ni kaimu mkuu wa utawala JKT amesema lengo la kuwekeana saini ni kuhakikisha Taifa linajitosheleza kwa chakula na kulipunguzia Taifa mzigo.


“Jeshi la kujenga Taifa JKT limeweka nguvu kubwa katika vikosi vyake kwani mazao yote ya kimkakati  yanalimwa Katika vikosi hivyo”


Aidha amebainisha  changamoto wanazokumbana nazo katika Kilimo ni mabadiliko ya tabia nchi, upungufu wa maabara ya kupima udongo ili ilete matokeo kwa uharaka na uhaba wa pembejeo za kilimo  pamoja na ukosefu wa Rasilimali Fedha.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya amesema makubaliano hayo yalikua ni ndoto yake ya kila siku kwani yeye ni mfatiliaji mkubwa katika shughuli wanazo fanya JKT.


kukutana kwa jeshi la kujenga Taifa JKT na wizara yakilimo kwa kutia saini ni moja wapo ya Malengo Makubwa  kwani JKT shughuli za kilimo wanazo fanya zinajulikana katika sekta ya kilimo nchini.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »