MHE. HEMED AITAKA JAMII KUJENGA MSIMAMO WA PAMOJA KATIKA KUPINGA VITENDO VYA UDHALILISHAJI

MHE. HEMED AITAKA JAMII KUJENGA MSIMAMO WA PAMOJA KATIKA KUPINGA VITENDO  VYA UDHALILISHAJI

Jamii nchini imeshauriwa kuwa na msimamo wa pamoja katika kupinga vitendo vya udhalilishaji vilivyoshamiri ndani ya visiwa vya Zanzibar ili kupunguza machungu kwa waathika wa vitendo hivyo wakiwemo wanawake na watoto. Makamu wa Pili wa Pili wa Rais Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ametoa ushauri huo mara baada ya kukamilika kwa ibada ya sala ya Ijumaa

Jamii nchini imeshauriwa kuwa na msimamo wa pamoja katika kupinga vitendo vya udhalilishaji vilivyoshamiri ndani ya visiwa vya Zanzibar ili kupunguza machungu kwa waathika wa vitendo hivyo wakiwemo wanawake na watoto.


Makamu wa Pili wa Pili wa Rais Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ametoa ushauri huo mara baada ya kukamilika kwa ibada ya sala ya Ijumaa katika Masjid ya Al-Twarika katika kijiji cha Karange Donge wilaya ya Kaskazini “B” Mkoa wa Kaskazini Unguja.


Mhe. Hemed ameleza azma ya seriakli ya awamu ya nane imelenga kuvitokomeza vitendo hivyo ambapo hivi karibuni imechukua jitihada za maksudi kwa kuifanyia marekebisho sheria ya makosa ya udhalilishaji kwa lengo la kuondoa mianya ya kupatiwa dhamana watendaji wa makosa hayo.

Nae ghatibu alietoa hutoba katika mskiti huo Ustadi Haji Ali Makame amewanasihi waumini kutimiza wajibu wao kwa kundelea kushikama na kushirikiana katika kuzidisha mapenzi miongoni mwao ili kupata matunda mema hapa duaniani na kesho  Akhera.


Mapema, Mhe. Makamu wa Pili wa Raisi alifika nyumbani kwa Mzee Ali Ameir kumjulia hali na kubadilisha nae mawazo.

Katika mazungunzo yao Mzee Ali Ameir amemuomba Makamu wa Pili wa Rais kumfikishia salamu zake za dhati za kumpa Pole Mhe. Rais kwa kuondokewa na Makamu wake wa kwanza Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad. 

Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)Febuari 26, 2021.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »