JESHI LA POLISI LADAIWA KUMPIGA RISASI KIJANA

JESHI LA POLISI LADAIWA KUMPIGA RISASI KIJANA

Na Mwandishi wetu , MBEYA  KIJANA Ivan Kabambala  mwenye umri wa miaka (17) Mkazi wa Kagera katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya, amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya  baada ya kudaiwa  kupigwa risasi  mgongoni na  Askari wa Jeshi la Polisi. Akizungumzia tukio hilo, baba mzazi wa marehemu, Aggrey Kabambala,

Na Mwandishi wetu , MBEYA

 KIJANA Ivan Kabambala  mwenye umri wa miaka (17) Mkazi wa Kagera katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya, amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya  baada ya kudaiwa  kupigwa risasi  mgongoni na  Askari wa Jeshi la Polisi.

Akizungumzia tukio hilo, baba mzazi wa marehemu, Aggrey Kabambala, amesema  limetokea majira ya saa mbili usiku  katika eneo ambalo marehemu alikuwa anafanya kazi ya kuosha magari

Baba Mzazi wa Marehemu Aggrey Kapamba

Baadhi ya wananchi wa Mtaa wa Kagera wamelalamikia kitendo hicho na kudai kuwa Jeshi la Polisi linahatarisha usalama wao.

Mwananchi wa Mtaa wa Kagera Clement Mgala
wananchi wa Mtaa wa Kagera

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, William Ntinika  ametoa    pole kwa familia ya marehemu Ivan  na kuwaomba wananchi wa Mtaa wa Kagera kuwa watulivu wakati wakisubiri  ukweli wa tukio hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, William Ntinika

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei,  amesema   marehemu Ivan ni miongoni mwa vijana  20 waliokuwa  wakipanga  njama za kufanya uhalifu   na kwamba baada ya kupata taarifa Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei
Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »