SIMANZI ZATAWALA MAZISHI YA NAIBU MKURUGENZI WA TARILI NA MKEWE

SIMANZI ZATAWALA MAZISHI YA NAIBU MKURUGENZI WA TARILI NA MKEWE

Mamina ya waombolezaji wamejitokeza katika mazishi ya aliyekuwa Maimu Mkurugenzi Taasisi ya utafiti wa mifugo na mtaalamu wa masuala ya uzalishaji wa wanyama (Tarili)  kanda ya kati marehemu Dkt Harun Chawala na mkewe Dkt Neema Mwasanganga yaliyofanyika katika kijiji cha Lundamatwa wilayani kilolo mkoani iringa ambapo miili ya marehemu hao wawili mume na mke wamezikwa


Mamina ya waombolezaji wamejitokeza katika mazishi ya aliyekuwa Maimu Mkurugenzi Taasisi ya utafiti wa mifugo na mtaalamu wa masuala ya uzalishaji wa wanyama (Tarili)  kanda ya kati marehemu Dkt Harun Chawala na mkewe Dkt Neema Mwasanganga yaliyofanyika katika kijiji cha Lundamatwa wilayani kilolo mkoani iringa ambapo miili ya marehemu hao wawili mume na mke wamezikwa March 8 2021 kijijini hapo.


Waombolezaji hao wamesikitishwa na kifo cha Dkt chawala na mkewe waliofariki dunia March 5 2021 kwa kufa maji baada ya gari lao aina ya Nissan xtrae T 483 BRR kusombwa na maji katika daraja la Shabani Robert  katika mto kikombo wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma. 


Waombolezaji hao wamesema walipokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa kwakuwa walikuwa wakiwafahamu marehemu hao kwa ucheshi wao na upendo wao waliokuwa nao pindi wanapokuwa kijijini hapo kwa nyakati tofauti tofauti waendapo kijijini.


Akitoa salamu za rambirambi za serikali katibu tawala wilaya ya mpwapwa Bi Sarah John Komba amesema tukio hilo liliwastua watu wengi kwa kuondokewa na watumishi hao kwa kufa maji baada ya gari lao kusombwa na maji wilayani Mpwapwa.


“Mimi Kama mwakilishi wa serikali niwape pole wazazi wote pande  mbili kuondokewa na watoto wenu nafahamu mliwapenda sana ila mwenyezi mungu amewapenda zaidi kubwa sasa hapa ni kuendelea kuwaombea katika sala zetu za kila siku huko waliko wataishi kwa amani na upendo Kama walivyokuwa na tutulie katika kipindi hichi kigumu cha majonzi maana kuondokewa na chawala na neema ni pigo kubwa na wameacha watoto wawili wadogo hivyo tuwaombe hawa watoto pia Waweza kuwa na afya bora katika kipindi hichi ambacho wamebaki kuwa yatima ila Sisi tutaendelea kuwatunza”amesema Sarah Komba.

Aidha Komba amesema Serikali imepoteza nguvu kazi kubwa kwa kuwa walikuwa bado vijana na wenye nguvu na wasomi wazuri ambao mchango wao ulikuwa mkubwa kwa serikali hakika watakubukwa kwa mema na mazuri waliyoyatenda kwa jamii ya mpwapwa na taifa kwa ujumla.


Katika mazishi hayo yaliyoongozwa na Katibu Tawala Wilaya ya Mpwapwa Bi sarh John Komba na Mkurugenzi wa tafiti na ugani kutoka Wizara ya Mifugo yaliyofanyika leo March 8 2021 katika kijiji cha Lundamatwa wilayani kilolo mkoani iringa yaliuzuriwa na wazazi wote wa familia mbili ya Chawala na Mwasanganga Ndugu jamaa mamia ya waombolezeji waliojitokeza kuwazika wapendwa hao Mr and Mrs Dkt chawala.

Na Barnabas Kisengi

Kilolo iringa March 8, 2021

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »