Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linawashikilia watuhumiwa 23 wa matukio mbali mbali ikiwemo wizi

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linawashikilia watuhumiwa 23 wa matukio mbali mbali ikiwemo wizi

LNa Scolastica Msewa, Kibaha. Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linawashikiria watuhumiwa 23 wa matukio mbali mbali ikiwemo wizi wa vitu mbali mbali vilivyoibiwa msibani baada ya kupuliziwa dawa wafiwa  huko Mlandizi mjini Kibaha. Akizungumzia na waandishi wa habari mjini Kibaha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, ACP Wankyo Nyigesa amesema tukio hilo la wizi

LNa Scolastica Msewa, Kibaha.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linawashikiria watuhumiwa 23 wa matukio mbali mbali ikiwemo wizi wa vitu mbali mbali vilivyoibiwa msibani baada ya kupuliziwa dawa wafiwa  huko Mlandizi mjini Kibaha.


Akizungumzia na waandishi wa habari mjini Kibaha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, ACP Wankyo Nyigesa amesema tukio hilo la wizi uliofanyika msibani baada ya mazishi watu wakiwa wamelala ndani wezi walivunja mlango wa nyumba wafiwa wakiwa wamepuliziwa dawa ndipo wezi wakaiba vitu mbali ikiwemo Televisheni tatu, mbili aina ya Startimes inch 32 na moja  aina ya UK inch 21,Simu za mkononi tano. (Tecno 3, Itel 01, Bontel 1).  


Alivitaja vitu vingine vilivyoibiwa msibani kuwa ni pamoja na Radio mbili aina ya SonnySpika nne, Deki mbili. Moja aina ya LS na nyingine aina ya HITACHKing’amuzi kimoja aina ya Startimes.
Kamanda Wankyo amesema Jeshi hilo limefanya operesheni kwa kipindi cha wiki moja kuanzia tarehe 01/03/2021 hadi tarehe 10/03/2021 katika Wilaya zote  tano za Polisi ambapo Watuhumiwa wengi kati ya hao 23 walikamatwa huko mlandizi wilayani Kibaha.


“Madhumuni ya misako hiyo ilikuwa ni kudhibiti na kuzuia matukio ya makosa ya wizi, Uvunjaji na  matumizi ya madawa ya kulevya” alisema Wankyo.
Katika operesheni hii tumefanikiwa kukamata  Watuhumiwa hao walikamatwa na vitu vingine mbalimbali  kama Bhangi kilo 296, Miche ya bhangi iliyokutwa imelimwa nyumbani kwa mtuhumiwa katikati ya  shamba la mahindi àmbapo mtuhumiwa alikuwa akitunza kwa kupalilia bhangi hizo sawa zao lake la mahindi na pia alikuwa na Mirungi bunda 35 huko wilayani Bagamoyo.


“Laini 74. Kati ya hizo laini 56 ni mpya na laini 18  zinazotumika kufanya utapeli zikiwa  zimesajiliwa kwa jina moja la Mosses Cosmas” alisema Wankyo.
Aidha Scanner moja aina ya Mantra kwa ajili ya kuchukua alama za vidole (Finger print)Mashine ya kusajilia lainiSolar power, Makoti 12 ya Kampuni ya ulinzi ya SGA, Pikipiki moja aina ya SAN LG nyekundu yenye namba za usajili T.659 CCA Ikiwa ni pamoja na Pombe ya gongo lita 49.


Hata hivyo kamanda Wankyo amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linawahakikishia wananchi kuwa linaendelea kuimarisha ulinzi na usalama wakati wote na operesheni hizi ni endelevu. 


Alisema Watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.
“Wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili wachukuliwe hatua za kisheria na kuufanya Mkoa wa Pwani kuendelea kuwa shwari” alisema Wankyo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »