Watanzania watatu waingia matatani kwa kusafirisha vinyonga na nyoka

Watanzania watatu waingia matatani kwa kusafirisha vinyonga na nyoka

Serikali inawashikilia Watanzania watatu kwa tuhuma za kushirikiana na raia wa Jamhuri wa Czech kusafirisha nje ya nchi vinyonga 74 na nyoka sita kinyume na sheria.Akizungumza na vyombo vya habari leo Alhamisi Machi 11, 2021 mkoani Iringa, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amesema vinyonga na nyoka hao walikamatwa na maofisa wa forodha


Serikali inawashikilia Watanzania watatu kwa tuhuma za kushirikiana na raia wa Jamhuri wa Czech kusafirisha nje ya nchi vinyonga 74 na nyoka sita kinyume na sheria.
Akizungumza na vyombo vya habari leo Alhamisi Machi 11, 2021 mkoani Iringa, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amesema vinyonga na nyoka hao walikamatwa na maofisa wa forodha wa Austria wakiwa wamewekwa kwenye begi huku wakiwa wamefunikwa kwa soksi na vifungashio vya plastiki.
Amebainisha kuwa uchunguzi bado unaendelea sehemu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kubaini namna vinyonga na nyoka hao walivyopitishwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) bila kugundulika.

Amesema watuhumiwa watakaobainika kuhusika na uhalifu huo wataunganishwa na wenzao ambao tayari wamekamatwa.
Kuhusu watuhumiwa hao, amesema wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kesho Ijumaa akidai watashtakiwa kwa makosa ya kusafirisha nje wanyamapori hao bila kibali, uhujumu uchumi pamoja na utakatishaji wa fedha kupitia biashara hiyo.
Dk Ndumbaro amesema vinyonga na nyoka hao waliokamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Vienna nchini Austria, inadaiwa wametoka Tanzania katika Milima ya Usambara ambako kuna aina mbalimbali za vinyonga.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro


Akizungumzia jinsi watuhumiwa hao walivyowanaswa, Dkt. Ndumbaro amesema baada ya kupata taarifa kupitia mitandao ya kijamii, wizara kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama na kwa kutumia kikosi kazi Taifa dhidi ujangili iliunda kikosi maalum cha kuchunguza tukio hilo.
Amesema kupitia taarifa za kiintelijensia, kikosi maalum kilifanikiwa kupata jina la mtuhumiwa aliyesafirisha vinyonga hao ambaye ni raia wa Jamhuri ya Czech.
Pamoja na juhudi hizo, Waziri Ndumbaro amesema Serikali ya Tanzania itashirikiana na nchi ya Austria katika uchunguzi unaoendelea ikiwa ni pamoja na kuwarudisha Tanzania vinyonga pamoja na nyoka hao.


Amesema Serikali itawasiliana na Jamhuri ya Czech ili watuhumiwa hao ambao ni raia wa nchi hiyo wachukuliwe hatua.
Wakati huohuo, Dkt. Ndumbaro amesema Serikali inakusudia kuifuta biashara ya wanyamapori hai ambayo ilizuiwa tangu Mei 2016.
Amesisitiza kuwa hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kufanya biashara ya wanyamapori hai ndani na nje ya nchi na mtu yoyote atakayebainika kufanya biashara hiyo wakati imezuiliwa atachukuliwa hatua kali za kisheria

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »