VIJANA WATAYARISHWE JUU YA SOKO LA AJIRA WANGALI VYUONI

VIJANA WATAYARISHWE JUU YA SOKO LA AJIRA WANGALI VYUONI

NA SALEH RAMADHANI DODOMA, MACHI 13.2021. Imeelezwa kuwa kila Mwaka  kati ya vijana 50,000 na 60,000 tu miongoni mwa vijana milioni moja wanaoingia kwenye soko la ajira kila mwaka ambao hubahatika kupata ajira kwenye sekta rasmi. Hayo yamebainishwa  jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi inayojihusisha na masuala ya utafiti wa namna ya kupunguza umaskini Tanzania (

NA SALEH RAMADHANI DODOMA, MACHI 13.2021.

Imeelezwa kuwa kila Mwaka  kati ya vijana 50,000 na 60,000 tu miongoni mwa vijana milioni moja wanaoingia kwenye soko la ajira kila mwaka ambao hubahatika kupata ajira kwenye sekta rasmi.

Hayo yamebainishwa  jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi inayojihusisha na masuala ya utafiti wa namna ya kupunguza umaskini Tanzania ( REPOA) Dkt. Donald Mmari wakati wa uzinduzi wa vitabu viwili  vya Taasisi hiyo vinavyohusu masuala ya vijana na wanawake.

Dk Mmari  amebainisha kuwa kutokana na hali hiyo zaidi ya vijana 900,000 hujaribu kujiajir,kuingia kwenye sekta isiyo rasmi au kuendelea kutafuta ajira huku wanaoingia kwenye sekta isiyo rasmi hupata ajira fupi zenye kipato kisichoaminika na kisichokidhi mahitaji yao.

“Ajira zao huwa kwenye mazingira duni ya kazi zisizo na mikataba,hivyo kupitia vitabu hivi vijana na wanawake wataongeza uelewa na kujiamini,”Amesema

Aidha amevitaja vitabu hivyo vilivyozinduliwa ni “Mpito wa Vijana kutoka Kazi kwenda Shule Tanzania,” na “Kuwawezesha Wanawake Nchini Tanzania katika muktadha wa Mageuzi ya Sera ya Jamii ya Kisasa” vimezinduliwa  kwa lengo la kuwapa hamasa vijana na wanawake Kuwa na utayari wa kujisimamia wenyewe kiuchumi na kijamii.

Dkt.Mmari amesema,vitabu hivyo vitasaidia kuleta uelewa na kuwapunguzia vikwazo kwenye ulimwengu wa ajira ili kuongeza tija na ufanisi Katika kazi zao kulingana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia.

wakati wa utekelezaji wa utafiti huo, Taasisi hiyo  ilifanya kazi na wadau tofauti na taasisi za serikali kwenye maeneo hayo ili kuwainua wanajamii kutoka Katika umasikini na Kuwa Katika kundi lenye matumaini ya hali nzuri kiuchumi.

“Matokeo ya utafiti huu yalisambazwa kupitia warsha na mapendekezo yaliyotolewa kwa taasisi zinazohusika kuwezesha uundaji wa sera za ushahidi na kuarifu mikakati anuwai ya maendeleo, “amesema Dk Mmari

kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za umma, Naghenjwa Kaboyoka ambaye alimwakilisha spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amesema suala la utafiti kwa sasa ni bado lina changamoto kubwa jambo linalopaswa kutiliwa mkazo zaidi .

Kutokana na hali hiyo ametoa wito kwa taasisi na wadau wengine kuzingatia eneo hilo ili kufanya tafiti mbalimbali zitakazosaidia kuibua changamoto zilizopo kwenye jamii ikiwa ni Pamoja na kuzipatia ufumbuzi.

“Utafiti bado ni shida kubwa, sio kwa madaktari tu au hata walimu,Kwa jumla eneo hilo linahitaji suluhisho la kudumu,tunahitaji ubunifu zaidi Katika suala hili,sote tunafahamu kuwa tafiti ni ni maendeo,” amesema.

Sambamba na hayo uelewa wa kutosha juu ya hali halisi kuhusu mazingira ya soko la ajira ni muhimu katika kuwatayarisha vijana juu ya matumaini yao na kupunguza muda wa kutafuta kazi baada ya kuhitimu masomo yao.


Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »