WAKRISTO WAASWA KUENDELEA KUWA NA IMANI NA MIUJIZA YA YESU KRISTO KATIKA KUFANISHA MASUALA MBALIMBALI YAKIWEMO YA KIROHO

WAKRISTO WAASWA KUENDELEA KUWA NA  IMANI   NA  MIUJIZA YA YESU KRISTO KATIKA KUFANISHA MASUALA MBALIMBALI YAKIWEMO YA KIROHO

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma. Wakristo wameaswa kuendelea kuwa na imani ya miujiza ya Yesu Kristo katika kufanikisha masuala mbalimbali ikiwemo ya kiroho. Wito huo umetolewa jana Machi,13,2021 jijini Dodoma na Dkt.Hery Mhando katika ibaada kuu ya Sabato kanisa la Waadventista Wasabato Kizota iliyokutanisha mitaa miwili ya Kizota na Chang’ombe. Dkt.Mhando amesema kuwa katika Zaburi 91 imesheheni  

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Wakristo wameaswa kuendelea kuwa na imani ya miujiza ya Yesu Kristo katika kufanikisha masuala mbalimbali ikiwemo ya kiroho.

Wito huo umetolewa jana Machi,13,2021 jijini Dodoma na Dkt.Hery Mhando katika ibaada kuu ya Sabato kanisa la Waadventista Wasabato Kizota iliyokutanisha mitaa miwili ya Kizota na Chang’ombe.

Dkt.Mhando amesema kuwa katika Zaburi 91 imesheheni   mibaraka na miujiza mbalimbali hivyo inalipa kutegemea Miujiza ya Yesu Kristo kwa maisha ya kila Siku.

DKT MHANDO, MIUJIZA

Aidha,Dkt.Mhando ametoa wito kwa washiriki kufanya maombi mara kwa mara pamoja na  kuhamasisha kualika wageni katika ushiriki wa mahubiri ya Satelite ya Kizota Net Event yatakayoanza Mwezi Juni Mwaka huu  huku mnenaji mkuu  ni Askofu mkuu wa kanisa la Waadventista Wasabato  Jimbo kuu la Kusini mwa Tanzania Mchungaji Mark Walwa Malekana.

Hali kadharika   Dkt.Mhando ametoa hamasa kwa washiriki  kuwa na desturi ya kuamka mapema kila siku .

Kwa upande wake Mchungaji Mafunzoni kutoka Chuo kikuu cha Uchungaji Bugema Uganda Mch.Samson Bucha amesema ni vyema kutumia muda mwingi kumtumikia Mungu na si kupoteza muda kumtumikia shetani kwani shetani analeta vitu vikuu viwili kwa mwanadamu ambavyo ni changamoto na ofa na anapoleta ofa  sio kwamba ana upendo bali ni kwa ajili ya kurubuni.

Mch.Samson Bucha

Kwa upande wao baadhi ya washiriki waliohudhuria katika Ibaada hiyo wamesema mahubiri ya leo yamekuwa na mibaraka tele katika maisha yao.

WASHIRIKI

Sabato ya jana Jumamosi Machi 13, 2021 katika kanisa la waadventista Wasabato Kizota imekutanisha mitaa miwili ya Chang’ombe na Kizota  ikihusisha takriban makanisa  nane  yakiwemo Veyula  SDA,Nguzo mbili SDA,Miyuji,SDA,Lugala SDA,Nala SDA,Kizota SDA,Chang’ombe SDA,Ndachi SDA .

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »