IMANI POTOFU BADO KIKWAZO UPATIKANAJI WA HAKI KWA WENYE ULEMAVU NA JAMII KWA UJUMLA

IMANI POTOFU BADO KIKWAZO UPATIKANAJI WA HAKI KWA WENYE ULEMAVU NA JAMII KWA UJUMLA

Na Barnabas Kisengi-Dodoma WADAU wa Elimu Jumuishi mkoani Dodoma wamesema kuwa mila na desturi za imani potofu bado zinaendelea kufanywa kwa watoto wenye ulemavu na wanajamii,hali ambayo  inayowakosesha  kupata haki zao za kimsingi kama ilivyo kwa wengine. Baadhi ya haki hizo ni wanazokosa ni pamoja na elimu,matibabu,miundombinu rafiki,burudani,nafasi za uongozi, katika kutoa maoni yao, na

Na Barnabas Kisengi-Dodoma

WADAU wa Elimu Jumuishi mkoani Dodoma wamesema kuwa mila na desturi za imani potofu bado zinaendelea kufanywa kwa watoto wenye ulemavu na wanajamii,hali ambayo  inayowakosesha  kupata haki zao za kimsingi kama ilivyo kwa wengine.

Baadhi ya haki hizo ni wanazokosa ni pamoja na elimu,matibabu,miundombinu rafiki,burudani,nafasi za uongozi, katika kutoa maoni yao, na kunyimwa fursa mbalimbali za kuweza kuchangia kwenye mijimuiko ya watuikiwemo kwa upande wa familia wanazoishinazo na katika mikusanyiko ya mikutano.

Wadau hao wamesema hayo wakati alipokuwa wakizungumza kwenye mafunzo ya mradi wa Elimu Jumuishi ulio chini ya Kanisa la FPCT kwa ajili ya viongozi wa Asasi za kiraia juu ya ushawishi na utetezi kwa watoto wenye ulemavu iliyofanyika Dodoma.

Richard Mwaga kutoka shirika lisilo la kiserikali la Afnet alisema kuwa bado kuna mila za Imani potofu miogoni mwa wanajamii zinazowanyima haki kwa watoto wenye ulemavu hali ambayo inayowasababishia  kuendelea kuteseka kuwa tegemezi kila siku kwenye maisha yao.

Amesema kuwa bado kuna umuhimu na ulazima kwa upande wa serikali na asasi mbalimbali watu binafsi , kutoa elimu kwa wanajamii na familia wanazoishi watoto hao ili kuwakomboa na waweze kupata haki zao za kimsingi ikiwemo elimu pamoja na mahitaji yao muhimu.

Kwa upande wake Erick Mapunda kutoka Tanzania Cheshira Foundation amesema kuwa watoto wenye ulemavu wana uwezo kubwa wa kuongeza uchumi kwa Taifa,ikiwa watapatiwa fursa mbalimbali za kuwezeshwa kielimu.

Amesema kuwa kwa kushirikiana familia,serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali kuna uwezekano mkubwa wa kuwafanya watoto hao kujisimamia wenyewe kwenye sekta mbalimbali ikiwepo katika kusimamia familia zao na maeneo ya serikalini tofauti na jinsi wanavyojengewa na Imani potofu kuwa wao hawawezi.

Naye Mwanasheria wa kujitegemea Fredrick Mkatambo amesema kuwa  watu wenye ulemavu wanapaswa kupewa fursa sawa katika masuala yote ya kimaisha kama ilivyo kwa wengine.

Mkatambo akizungumza kwenye mafunzo hayo ya ushawishi na utetezi wa elimu jumuishi,alisema kuwa kuna umuhimu wakutenga masuala  ya watu wenye ulemavu pamoja na kuwajumuisha na jamii ya kawaida ili waweze kupata haki hao hizo za kimsingi .

Amesema kuwa kwa upande wa watoto wenye ulemavu ni vizuri nao wakapata haki sawa na wengine hasa katika upatikanaji wa elimu wa mahitaji mengine tofauti na ilivyo kwa hivi sasa bado walio wengi hawapatiwi fursa zao zinazostahili kama wanadamu.

Amesema nchi nyingi duniani zimekuwa zikizungumzia misingi ya haki za binadamu ikiwa na maana ya kwamba wote  wana haki ya kuwa huru, hivyo ni muhimu kujali maslahi yao mapana ya watoto wenye ulemavu ili waweze kufurahia katika kupata elimu kama watoto wengine.

‘’hata kwenye shule zetu tunatakiwa kuzingatia maslahi mapana ya mtoto kujenga miundombinu sahihi,vyoo  rafiki hayo ndiyo maslahi mapana  kwa mtoto kwa mfano pale wilayani Bahi tunatengeneza chumba kimoja kwa ajili ya wasichana kujisitiri ili  wanapofika kwenye kipindi cha  hedhi wapate sehemu ya kujihifadhi ndiyo maslahi ninayosemea  hapaa’’alisema.

Mwanasheria huyo amesema kuwa kwa hapa kwetu nchini Tanzania iliweza kusaini na  kuridhia maazimio tofauti ya kimataifa ambayo hutoa usawa katika elimu kama vile mkataba wa umoja wa mataifa juu ya haki za watu wenye ulemavu 2006.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »