DODOMA: TARURA YATEKELEZA AGIZO LA MBUNGE, WANANCHI WAJITOKEZA KUSAMBAZA VIFUSI

DODOMA: TARURA YATEKELEZA AGIZO LA MBUNGE, WANANCHI WAJITOKEZA KUSAMBAZA VIFUSI

Na Barnabas Kisengi-Dodoma March 14, 2021 Ikiwa ni siku mbili tu baada ya Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mh Antony Mavunde na mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa chinyoya Bi Faustina Bendera na Diwani wa Kata ya Kilimani na wataalamu kutoka wakala wa barabara za mijini na vijijini TARURA kutembelea na kuona uharibifu mkubwa wa miundombinu

Na Barnabas Kisengi-Dodoma March 14, 2021


Ikiwa ni siku mbili tu baada ya Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mh Antony Mavunde na mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa chinyoya Bi Faustina Bendera na Diwani wa Kata ya Kilimani na wataalamu kutoka wakala wa barabara za mijini na vijijini TARURA kutembelea na kuona uharibifu mkubwa wa miundombinu ya barabara za mtaa huo wa chinyoya zilizoharibika vibaya kutokana na mvua za mwaka Jana na mwaka huu na kufanya mtaa huo kuwa kisiwa kutokana na vyombo vya usariri kushindwa kupita leo march 14 2021 majira ya mchana utekelezaji wa kutengeneza barabara hizo umeanza kutekeleza na tarula kwa kumwaga vifusi katika moja ya barabara hizo za mtaa ili zifunguke kwa kupita kwa magari.


Akizungumza katika eneo la barabara moja ambayo imemwagiwa vifusi na TARURA, Mwenyekiti wa mtaa huo Bi Faustina Bendera amemshukuru Mbunge kwa kutekeleza ahadi yake alioitoa juzi wakati akikagua miundombinu hiyo ya barabara za mtaa zilizoharibika kwa kiasi kikubwa
“Napenda kumshukuru mbunge kwa ahadi yake alio itoa juzi kuwa atatafuta vifusi na wataalamu wa tarula watatoa magari leo jumapili vifusi vimefika na hapa tunaendelea na zoezi la kuikarabati hii barabara moja ifunguke kwanza ili wananchi wa mtaa wangu waweze kupitisha vyombo vya usafiri ambavyo vilikuwa havipiti twakwibani miezi miwili sasa kufunguka kwa barabara hii kutaleta maendeleo hapa mtaani”amesema Faustna.


Aidha Mwenyekiti huyo amesema sasa hivi vifusi vilivyomwagwa na kusambazwe ni kwa muda tu ili shughuli za kiuchumi ziendelee kufanyika kwa kuwa TARURA walishasema wanasubiri mvua zikikatika ndio watakuwa na uwezo wa kuingiza mitambo na kuendelea na kuchonga barabara hizo za mtaa kwakuwa mtaa kwa sasa umeshapimwa na wananchi wanamiliki aridhi na viwanja kwa mtaa wangu.


Bi Faustina amewashukuru wananchi wa mtaa wake waliojitokeza kusaidiana kuhakikisha wamevisambaza vifusi hiyo vilivyoletwa na TARURA. Naye Mwenyekiti wa Chama Cha apMinduzi CCM tawi la Chinyoya amesaidiana kuongeza nguvu na kuwatia moyo wananchi waliojitokeza katika zoezi hilo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »