HABARI PICHA: WAZIRI SIMBACHAWENE AONGOZA KIKAO KAZI CHA KAMATI YA KUSIMAMIA, KUDHIBITI NA KURATIBU MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

HABARI PICHA: WAZIRI  SIMBACHAWENE AONGOZA KIKAO KAZI CHA KAMATI YA KUSIMAMIA, KUDHIBITI NA KURATIBU MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Na Barnabas Kisengi- March 15, 2021 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya kudhibiti na kusimamia mapato ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mh George Simbachawene leo Machi 15, 2021 amefungua kikao kazi cha kupitia taarifa ya kamati ya kusimamia,kudhibiti na kuratibu mapato na matumizi ya Wizara

Na Barnabas Kisengi- March 15, 2021


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya kudhibiti na kusimamia mapato ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mh George Simbachawene leo Machi 15, 2021 amefungua kikao kazi cha kupitia taarifa ya kamati ya kusimamia,kudhibiti na kuratibu mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa kipindi cha robo ya kwanza na ya pili ya mwaka wa fedha 2020/2021. Kikao kazi hicho kimefanyika jijini Dodoma. 


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia, Kudhibiti na Kuratibu Mapato na Matumizi ya Wizara, George Simbachawene, akizungumza katika kikao cha kupitia taarifa ya Kamati hiyo kwa robo ya kwanza na ya pili ya mwaka wa fedha 2020/2021, kilichofanyika jijini Dodoma, leo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio, na kulia ni Katibu wa Kamati, Jenitha Ndone.
Picha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia, Kudhibiti na Kuratibu Mapato na Matumizi ya Wizara, George Simbachawene (wapili kulia), akimsikiliza msoma taarifa ya Kamati ya Kusimamia, Kudhibiti na Kuratibu Mapato na Matumizi ya Wizara, Sunday Songwe, katika kikao cha kupitia taarifa ya Kamati hiyo kwa robo ya kwanza na ya pili ya mwaka wa fedha 2020/2021, kilichofanyika jijini Dodoma, leo. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio, na kulia ni Katibu wa Kamati, Jenitha Ndone. Picha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP), Suleiman Mzee akifafanua jambo katika kikao cha Kamati ya Kusimamia, Kudhibiti na Kuratibu Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kilichoongozwa na Waziri wa Wizara hiyo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, George Simbachawene (hayupo pichani), kilichofanyika jijini Dodoma, leo. Picha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia, Kudhibiti na Kuratibu Mapato na Matumizi ya Wizara, George Simbachawene (kulia), akizungumza katika kikao cha kupitia taarifa ya Kamati hiyo kwa robo ya kwanza na ya pili ya mwaka wa fedha 2020/2021, kilichofanyika jijini Dodoma, leo. Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio. Picha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Wajumbe mbalimbali wa Kamati ya Kusimamia, Kudhibiti na Kuratibu Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakimsikiliza Waziri wa Wizara hiyo, George Simbachawene (hayupo pichani), alipokuwa anazungumza katika kikao cha kupitia taarifa ya Kamati hiyo kwa robo ya kwanza na ya pili ya mwaka wa fedha 2020/2021, kilichofanyika jijini Dodoma, leo. Picha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »