WIZARA YA MIFUGO KUWAFUTIA LESENI WACHUNAJI NGOZI (+VIDEO)

WIZARA YA MIFUGO KUWAFUTIA LESENI WACHUNAJI NGOZI (+VIDEO)

Na MWANDISHI WETU,   MOROGORO WIZARA ya mifugo imesema itawachukulia hatua kali ikiwemo kuwafutia leseni zao wachunaji wa ngozi katika machinjio ya manispaa ya Morogoro wanaotoboa ngozi za mifugo na kuifanya kukosa thamani licha ya kupatiwa mafunzo na vitendea kazi Akizungumza mara baada ya kufanya ziara ya kukagua uzalishaji wa ngozi bora zinazohitajika katika soko, kaimu

Na MWANDISHI WETU,   MOROGORO

WIZARA ya mifugo imesema itawachukulia hatua kali ikiwemo kuwafutia leseni zao wachunaji wa ngozi katika machinjio ya manispaa ya Morogoro wanaotoboa ngozi za mifugo na kuifanya kukosa thamani licha ya kupatiwa mafunzo na vitendea kazi

Akizungumza mara baada ya kufanya ziara ya kukagua uzalishaji wa ngozi bora zinazohitajika katika soko, kaimu mkurugenzi msaidizi wa mazao ya mifugo, usalama wa chakula na lishe, Gabriel Bura alisema licha ya kufanyika mafuzo ya uchunaji bora wa ngozo lakini bado wapo watu wanao kiuta taratibu zilizowekwa

Alisema mafunzo yaliyotolewa yamesaidia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa ngozi bora lakini serikali haitawafumbia macho baadhi ya wachunaji wa ngozi wanaoendelea kutoboa ngozi kutokana na mahitaji makubwa yaliyopo hasa katika viwanda vikubwa vya ngozi zilivyoanzisha.

“tulizitoa lesei hizi kwa sharia ya ngizi namba 18 ya mwaka 2008, lakini pia tulitoa mafunzo ya uchunaji wa ngozi ili kuzipa thamani ngozi mnazozalisha lakini kuna baadhi yenu bado wanafanya makosa kwa kutoboa ngozi, sasa makosa haya yakijirudia tutawafutia leseni zao” alisema Bura

Aliongeza kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya rais Dkt John Magufuli imejidhatiti kwa kuanzisha na kufufua viwanda nchini ikiwemo kiwanda cha ngozi cha ACE Leather cha Morogoro na kiwanda cha ngozi kilichopo Moshi hivyo kitendo cha kuendelea kutoboa ngozi hizo ni kurudisha nyuma jitihada za serikali

Aliwataka wachunaji hao kuhakikisha wanaendelea kuzingatia sharia katika utendaji wa kazi zao sambamba na kutengeneza upya leseni zao ambazo zipo ukingoni kuisha muda wake wa kipindi cha mwaka mmoja ifikapo mwezi Agosti mwaka huu.

Joseph Kupa ni mkaguzi mkuu wa nyama manispaa ya Morogoro alisema kuwa pamoja na mambo mengine wanakabiliwa na changamoto ya baadhi ya watu kushindwa kufuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sharia sambamba na magonjwa ya ngozi

Alisema miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na baadhi ya wafugaji kuendelea kupiga chapa mifugo yao jambo linalosabisha ngozi kukosa thamani huku magojwa kama Exiima na Lab Skin ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakishambulia mifugo

“chagamoto tunazo pata mara nyingi ni migufo inakuja hapa ikiwa imepigwa chapa na mangine imeshambuliwa na magonjwa ya ngzo sasa ikifika hapa inakuwa tayari haina thamani hata hatuwezi kuichuna kwa sababu haiwezi kununuliwa na inatokana na baadhi ya wafugaji kutokuwa na elimu yakutosha juu ya umuhimu wa ngozi” alisema Kupa

Kwa upande wake mwenyekiti wa wachunaji wa ngozi katika machinjio ya manispaa ya Morogoro Mapinduzi Ernest alishukuru kwa elimu waliyoipata ambayo inawasaidia kwa kiasi kukibwa kuzalisha ngozi borana kuiomba serikali kufikisha elimu kwa wafugaji juu ya upigaji chama ili kubata ngozo bora.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »