MGOMO WA DALADALA WATIKISA MBEYA, RC ATOA TAMKO (+VIDEO)

MGOMO WA DALADALA WATIKISA MBEYA, RC ATOA TAMKO (+VIDEO)

Na Mwandishi wetu, MBEYA Wakazi wa Jiji la Mbeya, wamekumbwa na adha ya usafiri baada ya madereva wa magari ya kusafirisha abiria maarufu kwa jina la daladala kugoma kufanya kazi wakishinikiza Serikali kuziondoa bajaji kwenye Barabara Kuu. Mgomo huo umeanza alfajiri ya leo ambapo madereva daladala  wamesema  bajaji zinasababisha kazi yao kuwa ngumu na kuwapunguzia

Na Mwandishi wetu, MBEYA

Wakazi wa Jiji la Mbeya, wamekumbwa na adha ya usafiri baada ya madereva wa magari ya kusafirisha abiria maarufu kwa jina la daladala kugoma kufanya kazi wakishinikiza Serikali kuziondoa bajaji kwenye Barabara Kuu.

Mgomo huo umeanza alfajiri ya leo ambapo madereva daladala  wamesema  bajaji zinasababisha kazi yao kuwa ngumu na kuwapunguzia kipato kutokana na kuingilia njia zao kwa kuchukua abiria kwenye vituo vilivyotengwa kwa ajili ya daladala huku baadhi ya wananchi wakisema mgomo huo umeathiri shughuli zao za kiuchumi na kijamii.

Akizungumzia mgomo huo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amesema hawezi kuziondoa bajaji kwenye barabara kuu kwa sababu ni miongoni mwa vyombo vinavyoajiri vijana wengi kwa sasa.

Albert Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »