Na Saleh Ramadhani–Dodoma Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amesema wao kama mhimili wa Bunge wamepokea kwa masikitiko makubwa kuhusiana na kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ambapo amesema ni pigo kubwa kwa Watanzania kwani alikuwa shupavu na mpambanaji. Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Machi 18,2021
Na Saleh Ramadhani–Dodoma
Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amesema wao kama mhimili wa Bunge wamepokea kwa masikitiko makubwa kuhusiana na kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ambapo amesema ni pigo kubwa kwa Watanzania kwani alikuwa shupavu na mpambanaji.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Machi 18,2021 Spika Ndugai amesema Hayati Magufuli wakati wa uhai wake mambo mengi amesimamia ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu mbalimbali na Rais ni sehemu ya mhimili wa pili wa Bunge hivyo kamati zote za bunge zilizokuwa zimetawanyika katika ziara za kukagua maendeleo zimesitisha .
Aidha,Spika Ndugai amesema hotuba mbalimbali alizotoa Dkt.Magufuli zitaendelea kusimamiwa kwa manufaa ya watanzania .
Wakati huo huo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya chemba ambae pia ni Diwani wa Kata ya Mondo Saidi Sambala amesema Hayati Dkt.John Pombe Magufuli alikuwa mpenda watu na amewasaidia sana Watanzania kuzijua haki zao huku akisema watamkumbuka sana kwa mengi.
INSERT….. SAMBALA
kwa upande wake Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma na Mwenyekiti wa Taasisi za Elimu ya juu Tanzania Dkt Paul Loisulie amesema Hayati Rais Dkt John Magufuli enzi akiwa waziri wa ujenzi alikuwa ni mtu aliyependa kulisimamia jambo lake na kuhakikisha linakwenda kwa weledi hadi kukamilika kwake .
Hata hivyo JFIVE TV.COM imezunguka katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dodoma hususan sehemu za machinga na kuzungumza na mama mmoja ambaye hakutaka jina lake kutajwa amesema Rais Magufuli alikuwa mtu wa kujali machinga hali iliyosababishwa mama huyo ashindwe kujizuia na kuangua kilio.
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *