MAMA SAMIA SULUHU KURITHI NYADHIFA YA URAIS

MAMA SAMIA SULUHU KURITHI NYADHIFA YA URAIS

Mama Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa Makamu wa Rais toka mwaka 2015 sasa atakuwa mrithi wa rais John Magufuli ambaye amefariki Jumatano Machi 17. Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Tanzania kwa Rais kufariki akiwa madarakani, hivyo hakuna uzoefu wa nini kinafanyika katika hali kama hii. Kwa mujibu wa kifungu cha 37 (5)

Mama Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa Makamu wa Rais toka mwaka 2015 sasa atakuwa mrithi wa rais John Magufuli ambaye amefariki Jumatano Machi 17.

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Tanzania kwa Rais kufariki akiwa madarakani, hivyo hakuna uzoefu wa nini kinafanyika katika hali kama hii.

Kwa mujibu wa kifungu cha 37 (5) cha Katiba ya nchi hiyo iliyotungwa mwaka 1977, nafasi ya urais inapokuwa wazi kwa sababu yoyote ikiwemo kifo, viongozi watatu wameorodheshwa na ni Makamu wa Rais, na endapo hatakuwepo atachukua Spika wa Bunge na kama hayupo atachukua Jaji Mkuu.

Hivyo kwa mujibu wa katiba, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan ni rais mteule wa Tanzania.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »