VIONGOZI NA WANANCHI MAKAO MAKUU YA NCHI, DODOMA WAENDELEA KUMLILIA HAYATI MAGUFULI.

VIONGOZI NA WANANCHI MAKAO MAKUU YA NCHI, DODOMA WAENDELEA KUMLILIA HAYATI MAGUFULI.

Na Barnabas kisengi Dodoma  March 19 2021 Kufuatia kutangazwa kifo cha Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kilichotokea march 17 2021 majira ya saa kumi na mbili jioni jijini dar es salamu   wananchi na viongozi mbalimbali  Jijini Dodoma wameendelea kumlilia Hayati Magufuli. Naibu waziri ofisi ya Rais utawala bora menejimenti

Na Barnabas kisengi Dodoma 

March 19 2021

Kufuatia kutangazwa kifo cha Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kilichotokea march 17 2021 majira ya saa kumi na mbili jioni jijini dar es salamu   wananchi na viongozi mbalimbali  Jijini Dodoma wameendelea kumlilia Hayati Magufuli.

Naibu waziri ofisi ya Rais utawala bora menejimenti na utumishi wa umma   na utawala bora ,Deogratus Ndejembi ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la chamwino jijini Dodoma amesema wanachamwino na watanzania wamepokea kwa masikitiko makubwa kufuatilia kifo hicho cha Rais

Baadhi ya watumishi walioko mkoani Dodoma  akiwemo  mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Mpwapwa Julieth Mtuy,mdhibiti mkuu Ubora Elimu  wilaya ya Mpwapwa Grace Kamonga ,pamoja na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma na Mwenyekiti wa Taasisi ya Elimu ya juu Tanzania Dk. Paul Loisulie wamemwelezea  Hayati Magufuli alivyo iinua Dodoma na Tanzania kwa ujumla kwa utendaji wake wa kazi uliotukuka na uzalendo mkubwa kwa kuifanya Tanzania kuwa na amani na kufikia uchumi wa kati.

Mussa Mkunda ni mkazi wa Kata ya Kilimani mtaa chinyoya jijini Dodoma naye amepata fursa ya kumzungumzia Hayati Magufuli na kubainisha kuwa alikuwa   mtu wa watu.

Mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli utaagwa rasmi makao makuu ya nchi Dodoma Wiki ijayo siku ya jumatatu Machi,22,2021 kisha kusafirishwa Mwanza hadi Chato kwa ajili ya mazishi.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »