Ask. Masinga: Kifo cha Dk Magufuli kimetuondolea kiongozi aliyekuwa na malengo makubwa ya maendeleo kwa ajili ya wananchi wake

Ask. Masinga: Kifo cha Dk Magufuli kimetuondolea kiongozi aliyekuwa na malengo makubwa ya maendeleo kwa ajili ya wananchi wake

Na Mwandishi wetu Dodoma VIONGOZI wa madhehebu ya dini mkoani Dodoma wamesema kuwa kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli kilichotoke Jumanne tarehe 17/03/2021 ni sawa daraja lililokuwa linatumiwa na watanzania kwa ajili ya kujipatia maendeleo na sasa limekatika katikati ya mto na kuwarudisha nyuma watanzania kwenye umasikini. Askofu Mkuu

Na Mwandishi wetu Dodoma

Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli

VIONGOZI wa madhehebu ya dini mkoani Dodoma wamesema kuwa kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli kilichotoke Jumanne tarehe 17/03/2021 ni sawa daraja lililokuwa linatumiwa na watanzania kwa ajili ya kujipatia maendeleo na sasa limekatika katikati ya mto na kuwarudisha nyuma watanzania kwenye umasikini.

Askofu Mkuu wa Makanisa ya Philadelphia Gospel Assmbly Tanzania na nchi za East Africa Dk Yohana Masinga akizungumza na gazeti hili kwa upande wake, alisema kuwa kifo cha Dk Magufuli kimetuondolea kiongozi aliyekuwa amewawekea malengo makubwa ya ya maendeleo kwa ajili ya wananchi wake lakini kwa hivi sasa tunaona kama vile daraja lake la malengo limekatikia katikati ya mto na watanzania wameshindwa kuvuka.

Hata hivyo ikimbukwe kuwa kiongozi huyo alikuwa ametuongoza katika kumtumaini Mungu kwa vitendo kwa kila jambo kwa maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla hususah kwa watu wenye kipato cha chini.

Amesema Dk Magufuli tutaendelea kumkumba kwenye uongozi wake huo e kutokana na kipindi chote kwa kuwa alikuwa akimtanguliza Mungu mbele  kwanza siku zote za utendaji wake na kwenye maisha yake na kwa watanzania kwa wote.

Dk Masinga pia amewaomba viongozi waliopo madarakani na kwa watanzania kwa ujumla kuendeleza kuenzi yale yote aliyokuwa ameyafanya kwa ajili ya maendeleo ya Taifa hili huku tukiendelea kuombea amani na utulifu.

Kwa upande wake Shehe wa Mkoa wa Dodoma Mustaph Rajabu amesema kuwa ujanja na mafanikio ya miaka mitano ya uongozi wake wa Dk John Magufuli yalitokana na kumcha Mungu kwa uaminifu,na ndivyo wanavyotakiwa viongozi waliopo madarakani  kufuata nyayo zake hizo za kiutendaji tena kwa vitendo.

Shehe Rajabu amesema kuwa kwenye enzi zake za uhai Rais Magufuli alimtanguliza Mungu kwa kila jambo na ndiyo maana aliweza kufanikiwa kwa vitendo,ikiwepo kwa watumishi wake kuhakikisha kunakuwepo nidhamu ya hali ya juu ambapo iliyolifanya taifa hili kuheshimiwa na mataifa mbalimbali.

Hata hivyo shehe huyo amewataka watanzania kwenye kipindi hiki cha majonzi kuwa wavumilivu na kuondokana na utofauti wa aina yoyote kama vile kwenye suala la siasa,itikadi za vyama pamoja na Imani za kidini bali tusimame kwa pamoja na tuishi katika yale yaliyo mazuri aliyotuachia.

“Rais Dk Magufuli ametuachia mengi lakini lililokubwa ni hili la kumtanguliza Mungu kwa kila jambo ikifuatia nidhamu kwenye kazi kwa upande wa watumishi pamoja na kufanya kazi kwa bidi kwa ajili ya kuleta kipato kwa wananchi wake”amesema Sheh wa mkoa.

Askofu wa kanisa la International Sinai Ipagala Mkoa wa Dodoma Selvester Thadey,amesema kuwa kifo cha Rais wetu mpendwa Dk John Magufuli kimetuacha njia panda watanzania kutokana na jinsi alivyokuwa ametuthamini wananchi wake.

Rais Dk Magufuli kwenye utawala wake aliweza kugusa kila eneo bila kujali itikadi yoyote ile iwe ya vyama  vya siasa,dini,kabila au rangi wakubwa kwa wadogo,wote alitutumikia kama kiongozi anajali familia yake.

Hivyo kutokana na  kifo hiki tunatakiwa kuongana kwa pamoja kuhakikisha tunaiombea familia yake pamoja na Taifa ili amani iendelele kutawala na kwa wale viongozi wetu waliopo madarakani waweze kuendeleza maono ambayo aliyoyaanzisha kwenye utawala wake wa miaka mitato na ile ijayo pia.   

Naye Makamu Katibu Mkuu Taifa Kanisa la PHAM (T) Julias Bundala kwa upande wake amesema kuwa kuondokewa kwa kiongozi wetu jemedali ni pigo kwa watanzania kutokana na utendaji wake wa kazi alivyokuwa akiwajali wananchi wake wa hali ya chini na huku ukitimiza maono yake ya kubadilisha Tanzania kuwa nchi ya ulaya.

Askofu Bundala amesema kuwa ndani ya miaka 5 tayari Tanzania imeanza kubadilika kutokana na mafanikio mbalimbali ambayo yameanza kujitokeza,hivyo ni Imani yetu kwa watanzania wale wote watakaosimamia maendeleo hayo wahakikishe wanafanikisha kama ilivyokuwa kwenye fikra zake kwa ajili ya wananchi wa kitanzania.

“Hata hivyo pamoja na mafanikio hayo viongozi ambao watakaoendelea kufuata nyayo za Rais Dk Magufuli waendelee kusimamia uwepo wa kmakao makuu ya chama na serikali,ikiwemo na miradi mikubwa ambayo tayari imeanza kujengwa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa Tanzania”amesema Bundala

Aidha amewataka watanzania kuhakikisha kwa kipindi chote cha majonzi wanakuwa kwenye maombi kwa ajili kuliombea Taifa ili amani na mshikamo uendelee kudumu,na shetani asipate nafasi ya kutuingizia vitu visivyohitajika kwa Taifa la Tanzania.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »