IKIWA leo ni Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani baadhi ya Wadau mbalimbali wa Habari wametoa maoni yao kuhusiana na siku hii huku wakitoa pongezi kwa waandishi wa habari kutokana na kazi ambazo wamekuwa wakifanya katika kuhabarisha Umma na kutoa wito kuendelea kufanya kazi kwa weledi na kuwa wazalendo kwa kutanguliza mbele maslahi
IKIWA leo ni Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani baadhi ya Wadau mbalimbali wa Habari wametoa maoni yao kuhusiana na siku hii huku wakitoa pongezi kwa waandishi wa habari kutokana na kazi ambazo wamekuwa wakifanya katika kuhabarisha Umma na kutoa wito kuendelea kufanya kazi kwa weledi na kuwa wazalendo kwa kutanguliza mbele maslahi ya Nchi yao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Jfive hii leo wamesema kuwa Siku hii ni muhimu kwa Wandishi wa habari hivyo ni mambo mengi yanajadiliwa na Waandishi wa Habari kwa lengo la kusaidia kuboresha vyombo vya habari na utendaji kazi wa waandishi wa Habari.
Mmoja wa Wadau hao ni Mkuu wa Wilaya ya Igunga John Mwipopo amesema waandishi ndio kiunganishi cha wananchi na Serikali ni vyema kuwa wazalendo huku Mthibiti Mkuu Ubora wa Shule Wilaya ya Mpwapwa amesema Serikali imekuwa ikitoa nafasi kwa waandishi wa habari licha yakuwepo kwa changamoto mbalimbali huku akitaka kupunguzwa kwa adhabu kwa vyombo vya habari ambavyo vinafungiwa kutokana na kukiuka Sheria pamoja na ugumu wa upataji wa habari kwa waandishi Serikali iangalie hilo.
Naye Afisa Elimu kata ya Chamkoroma wilayani Kongwa Sifrasi Japhet Nyakupola amesema Serikali ivipe uhuru Vyombo vya Habari kufanya kazi katika kuibua masuala mbalimbali na mambo hayo yasifichwe katika kujenga uelewa wa pamoja ili kufikia uchumi wa kati .
Hata hivyo baadhi ya Waandishi wa habari nao walikuwa na haya yakusema.
Na. barnabas kisengi
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *