RAIS Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewashukuru Wananchi wa Mkoa Kaskazini Unguja kwa kuitikia wito na kujumuika naye katika futari Maalum

RAIS  Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewashukuru Wananchi wa Mkoa Kaskazini Unguja  kwa kuitikia wito na kujumuika naye katika futari Maalum

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewashukuru Wananchi wa Mkoa Kaskazini Unguja na Makundi Mbalimbali kwa kuitikia wito na kujumuika nae katika futari Maalum aliyowaandalia katika Mkoa huo. Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi, aliendelea na utaratibu wake wa kuandaa futari kwa ajili ya wananchi wa Mikoa mitano

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewashukuru Wananchi wa Mkoa Kaskazini Unguja na Makundi Mbalimbali kwa kuitikia wito na kujumuika nae katika futari Maalum aliyowaandalia katika Mkoa huo.

Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi, aliendelea na utaratibu wake wa kuandaa futari kwa ajili ya wananchi wa Mikoa mitano ya Zanzibar.

Katika hafla ya futari kwa Wananachi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja iliofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo ziliopo Mkokotoni, Dk. Mwinyi aliwashukuru wananchi wa Mkoa huo kwa kuitikia wito wake na kukutana pamoja kwa ajili ya futari, akibainisha kuwa  hilo ni jambo jema.

Aidha, aliwashukuru wananchi hao kutoka makundi mbali mbali kwa kumtunukia zawadi mbali mbali, jambo lililompa faraja kubwa na kuwaombea kheri kwa Mwenyezi Mungu.

Nae, Mkuu wa Mkoa huo, Ayoub Mohamed Mahamoud, alimshukuru Rais Dk. Mwinyi kwa uungwana wake wa kuamua kuwafutarisha wananchi wa Mkoa huo, pamoja na kumuomba kupokea zawadi mbali mbali kutoka kwao.

Abdi Shamna, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777476982. Fax: 024 2231822 

 E-mail: abdya062@gmail

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »