WAKAZI WA KAGERA WAHIMIZWA KUENDELEZA UTAMADUNI NA MICHEZO YA ASILI

WAKAZI WA KAGERA WAHIMIZWA KUENDELEZA UTAMADUNI NA MICHEZO YA ASILI

NA NYEMO MALECELA – KAGERA JAMII mkoani Kagera imetakiwa kuendeleza michezo ya asili ikiwamo majigambo ili kuwezesha kizazi cha sasa kufahamu asili na tamaduni zao. Akizungumza katika tamasha la majigambo maarufu kama ‘OKWEBUGA’ lililoandaliwa na serikali ya Mkoa wa Kagera kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa michezo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Profesa Faustine

NA NYEMO MALECELA – KAGERA

JAMII mkoani Kagera imetakiwa kuendeleza michezo ya asili ikiwamo majigambo ili kuwezesha kizazi cha sasa kufahamu asili na tamaduni zao.

Akizungumza katika tamasha la majigambo maarufu kama ‘OKWEBUGA’ lililoandaliwa na serikali ya Mkoa wa Kagera kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa michezo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Profesa Faustine Kamuzora amesema kuwa kwa Kagera utamaduni wa kujigamba umeanza kupotea.

Baadhi ya wasanii walioshiriki majigambo hayo kutoka katika Halmashauri za wilaya saba wameiomba serikali kutoa kipaumbele katika kuibua michezo ya zamani, maana mbali na kuburudisha pia ina mafundisho mbalimbali kwa jamii, huku Afisa Utamaduni Mkoa wa Kagera, Kefa Elias akidai mashindano hayo yanalenga kutoa hamasa kwa wasanii.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »